Kwa
kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi
zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu
salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka
mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi
mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa
ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.Hiki
ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga
ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi
huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na
kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.Kutokana
na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na
mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa
makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki
na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au
kutengeneza kile unachokihitaji.
VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.Kabla
ya kuanza kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa
kuanza kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa
hivyo ni kama vifuatavyo:-
UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.Eneo
ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu
mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa
mizinga, kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na
nyuki.Hivyo ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.
DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.Mabanda hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-
1. Kukinga mizinga na jua na mvua.Hii
ni sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga
mabanda ya kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia
mzinga kuweza kudumu kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki
kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki
hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani ya mzinga badala kutumia
muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.Nyuki
wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga
huamua kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu
nyingine.Hivyo nio vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza
kunyeshewa na mvua.Pia
mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda
mfupi, hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga
wako dhidi ya mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.2. Kukinga na wanyama waharibifuMabanda
haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga
kushindwa kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza
mashambulizi ya nyuki kwa viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda
na banda kufungwa milango.
3. Ulinzi na ukaguajiUjenzi
wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu
salama dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati
wa uangalizi wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga
hiyo huwa ni rahisi sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na
uwekaji wa kumbukumbu za kila mara.Pembeni
ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya
kutoka na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.
MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.Mizinga
ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata
makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama
ifuatayo:-1. Mzinga wa kibiasharaHuu
ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale
wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza
kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka
hadi mwaka.
Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-
A. Box la kuzalishia watoto wa nyukiNi
box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili
ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi
wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula. Box hili hutumika na
malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao
husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.Pia
box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili
ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha
nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika
brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha
kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.Kwa
kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa
misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya
kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti
tofauti vya mwaka na kuendelea.
B. Kitenga malikiaHiki
ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box,
wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa
lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile
la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi
kupanda kuelekea kwenye super box.
C. Box la kuhifadhia asaliHili
ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa
ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa
wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa
nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini
yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na
kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa
nyuki.Uvinaji
wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo
katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa
frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya
kisasa iitwayo Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza
asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.Mara
baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa
na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana
nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno
wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya
aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.
2. Mzinga wa viunziHuu
ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na
kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali
hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji,
isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa
viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha
mzinga huu.Mzinga
huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na
sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu
huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika
uvunaji wa asali hiyo.Uvunaji
wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na
kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa
kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.
Papai
ni moja ya tunda mashuhuli linatumika kwa kiasi kikubwa nchini
Tanzania. Pia tunda hili linaweza kuwa na faida mbali na afya, katika
kukuza uchumi wa mkulima wa zao hili. Pia linawezakuwa chanzo kikubwa
cha pesa za kigeni kwa kuuza nje ya nchi.Uzalishaji
wa papai nchini Tanzania ni kwa kiasi kidogo ukilinganisha na mahitaji
ya watumiaji, hivyo inahitajika nguvu zaidi katika uzalishaji wa zao
hili.
Kijinsia mpapai umegawanyika katika aina tatu.
- Mpapai wenye maua kiume tu.
- Mpapai wenye maua kike tu.
- Mpapai wenye maua ya jinsia zote (Hermaphrodite papaya).
Katika
uzalishaji kila aina ya mpapai unahitajika. Mpapai wenye maua ya kiume
uhitajika katika urutubishaji wa mpapai wenye maua ya kike ili kupata
matunda. Mpapai wenye maua ya jinsia zote hauhitaji mpapai wenye maua ya
kiume maana uweza kujirutubisha wenyewe.Kutokana
na jinsia ya maua mpapai huweza kutengeneza matunda yenye maumbo
tofauti. Matunda yanayotengenezwa kutoka katika mpapai wenye maua ya
kike tu huwa na umbo la mviringo zaidi au yenye umbo la yai na matunda
yanayotokana na mpapai wenye maua ya jinsia zote mbili huwa na umbo la
refu zaidi au umbo la pear.UZALISHAJI WA ZAO LA PAPAI.Miche ya mpapai Katika uzalishaji wa miche ya mpapai kuna aina mbili za mbegu ambazo huweza kutumika:1. Mbegu za Kawaida (Local seeds).Hizi
ni mbegu ambazo huweza kukusanywa toka katika mipapai ya kienyeji. Aina
hii ya mbegu ni vigumu kujua kati ya mbegu ni ipi dume, jike ama yenye
jinsia zote.Hivyo
itakulazimu kung'oa baadhi ya mipapai dume pindi itakapo weka maua
hivyo kuacha majike na yenye jinsia zote mbili. Mapapi yenye maua ya
kiume uachwa kwa uwiano wa 1:50 ya mipapai yenye maua ya kike.2. Mbegu chotara (Hybrid seeds)Aina
hii ya mbegu ni nzuri kwa sababu mbegu zote huwa ni ya mipapai nyenye
maua ya kike na ya kiume pamaja (Hermaphrodite papaya)na pia hukua
haraka na kutengeza miti mifupi yenye uzao mkubwa ukilinganisha na ile
ya kienyeji. Mfano. Red royolen F1 au MALAIKA F1.UPANDAJI.Panda
mbegu moja tu kwa kila kiriba chenye udongo uliochanganywa vizuri na
kujazwa robo tatu. Kisha weka viriba vyako venye mbegu chini ya kivuri
kisha mwagilia maji. Baada ya kumwagilia unaweza pulizia kiasi kidogo
cha kiuwatilifu (fungicide & Insecticide) kwenye udongo wako ili
kuzuia wadudu na fungasi wasiathili mmea wako.Mbegu
ya papai uweza chukua siku 8 hadi 15 kuchomoza toka kwenye udongo.
Hivyo hakikisha unamwagilia maji kila siku kwa kiasi. Usimwagilie maji
mengi sana. Mpapai huweza kuamishwa toka kwenye kitalu baada ya wiki
sita hadi nane.KITALU CHA MIPAPAI NA BAADHI YA SABABU MUHIMU ZINAWEZA ATHILI UKUAJI WA MIPAPAI.Mpapai
upendelea zaidi udongo unaopitisha maji na mzuko wa hewa kirahisi na
wenye makadilio ya Ph 6.5. Inapowezekana zuia kupanda mimea yako kwenye
udongo wa mfinyanzi na wenye magadi. Kiasi cha maji kilichopo kwenye
udongo huweza kuonyesha ukubwa wa matunda.Eneo
lenye udongo wenye unyevunyevu mwingi huweza tengeneza matunda makubwa
na yaliyoja maji maji na eneo lenye unyevunyeku kidogo hutengeneza
matunda madogo na magumu. Mpapai hawezi kuvumilia upepo mkali, maji
yaliotwama pamoja na ukame.
UANDAAJI WA SHAMBA.Njia
ya kuandaa shamba itategemea na eneo (topography), aina ya udongo,
vifaa vinavyotumika kuhudumia shamba. Nafasi kati ya mmea na mmea ni
mita 2 hadi 2.5 na kati ya mstari na mstari ni mita 2.5 hadi mita 3.Andaa
mashimo yenye upana na urefu wa sentimita 60. Tenga udongo wa chini na
wa juu. Kisha changanya udongo wa juu na mbolea ya samadi. Katika
kurushisha kwenye shimo tanguliza udongo ulochanganywa na mbolea ya
samadi chini na juu malizia na udongo uloutoa chini wakati wa kuchimba
shimo.Kiasi
cha mmea huwa kati ya 1000 hadi 2000 kwa hekta (400 hadi 800 kwa ekari)
Kupanda mimea shambani Baada ya hizo wiki sita hadi nane hamishia mimea
yako shambani. Kazi ya uhamishaji wa mimea ufanyika wakati wa asubuhi
sana, jioni ama kukiwa na mawingu ili kuzuia madhara ya jua kwa mimea.
UWEKAJI WA MBOLEA. Zuia
matumizi ya mbolea zenye chlorine maana mipapai uathiliwa na chlorine.
Wiki moja baada ya kuhamisha miche yako weka mbolea gramu 28 kwa kila
mche. Tumia mbolea yenye phosphate kwa kaisi kikubwa.Mfano; - 12:24:12.
(NPK) Baada ya hapo kila baada ya wiki mbili weka mbolea yenye Nitroni
kwa kiasi kikubwa kiasi cha gramu 56 kwa mmea. Mfano. 20:10:10 (NPK)
Potassium inahitajika kwa maua na kuweka matunda hivyo tumia mbolea
yenye potassium kiasi kikubwa mara baada ya kuona mmea wako umeanza
kuweka maua, kiasi cha gramu 114 cha mbolea huitajika, fanya hivyo kila
baada ya mwezi. Mfano. 12:12:17 + 2 (NPK) . Weka mbolea ya majani yenye
virutubisho vidogo vidogo ikiwemo boron kila mweze. Boron ni mbolea ya
muhimu katika kupata matunda mazuri.
UMWAGILIAJI.Maji
ni sehemu ya muhimu sana katika maisha ya mmea kwa kipindi chote. Maji
ni ya muhimu sana katika kuweka maua, matunda na ukuaji wa matunda.
Katika ukuaji wa matunda hakikisha unaweka lita 23 kwa kila mmea kwa
wiki.Magugu
Hakikisha unazuia magugu kipindi cha mwanzo ili kuzuia ushindani kati
ya mimea na magugu kwa virutubisho na maji. Na pia kuzuia magugu kubeba
vimelea na wadudu wanaoweza kuathili mazao yako.HATUA ZA UKUAJI WA MPAPAI.
- Kitalu - Wiki 1 - 6 -Hatua ya ukuwaji wa haraka baada ya kuamishiwa.
- Shamba - wiki 7 -16 -Maua na kuweka matunda.
- Wiki 17 - 21 -Kukua kwa matunda.
- Wiki 22 - 26 -Mavuno ya kwanza
- Wiki 37 -kuendelea Week 37 ni miezi tisa au kumi sio kwa hiyo kilimo cha mapapai huchukua miezi 10 kupata mavuno
GHARAMA
- Kununua ekari moja inategemea na eneo ulipo na bei husika.
- Kununua mbegu tsh 50,000-100,000.
- Kumwagilizia kila siku -upandaji -kuhamisha kutoka kwenye vitalu hadi kwenye shamba -machine ya kumwagilizia 1,500,000/-
- Generator tsh lak 6
- Mbolea tsh 100,000 kila mwez -na vibarua shambani -kulima kwa trekta 40,000 Gharama zote kama mil 3-4 hiv mpaka kuvuna.
MAVUNO NA FAIDA.Kama
umelima ekarI moja unaweza ukapata matunda 15- 35 kwa mvuno wa Kwanza
tu twende kimahesabu EkarI ina miche 400-800 Tuseme tupate miche 600 kwa
ekari, kila mche utoe matunda 20 chini kabisa 600×20=12,000.Matunda
Soko Kwa sasa unaweza ukauza kwa jumla jumla tsh 1500-3000 Tuuze kwa
bei ya chini 1500 kwa kila papai 12000×1500=18,000,000/- Ukitoa Gharama
za uendeshaji unaweza ukabaki na tsh 14,000,000 au toa 4,000,000 uweke
kwenye dharura unaweza ukamake tsh 10 mil kwa ekar moja tu.
Zao
hili pia hujulikana kwa jina la "Nyanya Chungu", "Ngogwe" au "Ntongo".
Huu ni mmea wa kitropiki, na kustawi kwake karibu ni sawa na bilinganya.Mmea
hukua na kufikia urefu wa meta moja hadi moja na unusu na matawi na
majani yake hufanya kichaka. Nyanya mshumaa zinaweza kuwekwa katika
makundi mawili: yaani aina itoayo matunda madogo madogo na machungu sana
na aina itoayo matunda makubwa na machungu kidogo.Rangi
ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyeupe, na
yakipevuka kabisa hugeuka mekundu. Matunda yafikia hatua ya kupevuka
huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda. Matunda
hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au huchanganywa na mboga
zingine. Pia hupikwa pamoja na ndi.
Kupanda:
Miche huoteshwa kwa kupanda mbegu ambayo husiwa kwenye kitalu na
kutunzwa kama mazao mengine. Miche ifikiapo kimo cha sentimeta 10 hadi
15 au majani manne 4 hupandikizwa bustanini , kwa umbali wa sentimita 50
kwa 75 au sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii kutegemeana na
ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya "Ngogwe" hutunzwa kama bilinganya,
huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa kutosha. Mazao huanza kuvunwa
miezi miwili baada ya kupandikizwa, na uvunaji huendelea kwa muda mrefu
kidogo.Maadui:
Nyanya Mshumaa ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa
maji kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na
baadhi ya Magonjwayasababishwayo
na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao
hushambulia zao hili, madhara ya si makubwa sana kiasi cha kutisha au
kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa
mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.Kuvuna:
Mboga huvunwa wakati zikiwa bado mbichi. Ili ziweze kukaa kwa muda
mrefu (hata majuma mawili) bila kuharibika, inapendekezwa kuzichuma
pamoja na sehemu ya vikonyo vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa
kuzitayarisha kupikwa. Kwa hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi
masoko ya mbali bila kuharibika.Mkulima ongeza uzalishaji katika mazao ya mboga mboga ukuze uchumi wako.
NB:
Umbali wa cm 50 kwa cm 75 ni mzuri sana kwa kuwa unaweza kupata mazao
mengi na kupunguza wingi wa magugu ukizingatia in cover crop ila lazima
uhakikishe ardhi yako ipo vizuri kwa rutuba maana matumizi ya mbolea ni
amakubwa.
Matikiti maji aina ya Sugar baby inachukua siku 60 tu kuvuna ukiongeza na siku 3-5 za kukaa ardhini, zao hili unaweza kulima mara 4 mwaka. Mfano ukiwa na ekari 5 kila eka moja inaweza kukuingizia Milioni 2 hadi 3.
Mambo muhimu- Nafasi inayotakiwa ni 2mm toka mmea mmoja kwenda mwingine
- Kila shimo unaweza weka mbegu 2 ambazo zinazaa matunda 2 hadi 3
- Kila shimo unaweza kupata matunda 4 hadi 6 ( wastani matunda 5).
- Kwa ukubwa wa ekari 5 unaweza kuwa na mashimo 1000 hadi 1200
- Idadi ya matunda: Mashimo x Matunda kwa shimo x ekari (1,000 x 5 x 5 = 25,000)
Mapato: wastani wa shilingi 500 kwa tikiti x idadi ya matikiti kwa eneo la ekari 5 (25,000 x 500 = 12,500,000)Mapato kwa mwaka: 12,500,000 x 4= 50,000,000Gharama za uendeshaji wa shamba ni Tsh 25,000,000Faida Kuu ni Tshs 25,000,000 Milioni.
Hii
ni aina ya mbuzi wa maziwa ambao asili yake ni uswizi katika eneo la
Obertoggenburg kama wanavyoitwa, hii ndio mbegu ya mbuzi wa maziwa wa
zamani zaidi kuliko zote. Kwa hapa Tanzania wanapatikana Uyole, SUA na
Tengeru (hivi vyote ni vyuo vya mifugo)
UZALISHAJIMbuzi
hawa wanauwezo wa kuzalisha maziwa wastani wa lita mbili kwa siku au
zaidi, hawatoi maziwa mengi kama Saanen ila maziwa yao yana kiasi cha
mafuta kati ya 3% - 4%
MAUMBILEMbuzi
hawa wana umbile la wastani lakini ni wakubwa kuliko mbuzi wa kienyeji,
kilo 55 kwa majike na kilo 75 kwa madume, wana rangi ya kahawia (khaki)
mpaka hudhurungi (brown) pia wana mistari miwili usni yenye rangi ya
maziwa au nyeupe kuanzia juu mpaka kwenye pua (kama duma) huwa na viwele
(udder) vikubwa na pia ni wazazi na walezi wazuri, mara nyingi huweza
kuzaa mapachaHALI YA HEWAMbuzi
hawa hawawezi kuhimili hali ya joto, bali hufanya vizuri kwenye maeneo
yanye baridi kama mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma, Njombe, Dodoma,
Singida n.k. Wanahitaji chakula chakutosha ili kutoa maziwa mengi, pia
chakula kiwe na virutubisho kamili. Ingawa pia wanaweza kuchungwa kwenye
maeneo yenye ukame kiasi na wakaweza kufanya vizuri (good foragers)
TABIAMbuzi
hawa huishi kwa makundi wakitoroka au kuingia kwenye shamba la mazao
basi huenda wote na hufundishika kirahisi sana hii husababisha urahisi
wa kuwafundisha kukamuliwa na mashine.