Inaelezwa kuwapo na tafiti zilizowahi kufanyika na kuchapishwa katika jarida lijulikanalo kwa jina la ‘Archieve’ la nchini India mnamo Oktoba 27 mwaka 2010, ambapo jarida hilo lilieleza kwamba juisi ya majani ya mpapai iliweza kusaidia wagonjwa watano waliowahi kupata homa ya dengue.
Mbali na utafiti huo, pia kuna tafiti zilizowahi kufanywa na madaktari wa nchini Marekani na Japani na kubaini kuwa, juisi ya majani ya mpapai ina uwezo wa kutibu malaria na saratani, japokuwa tafiti hizo hazikukubawaliwa kisayansi.
Faida za kiafya za tunda la papai
Aidha, wataalam wa lishe nao wanaeleza kwamba, watu wenye matatizo ya kupatwa na majipu, uvimbe na vidonda mara kwa mara huwa na upungufu wa virutubisho muhimu, ambavyo huweza kupatikana ndani ya papai, hivyo imegundulika watu wenye matatizo hayo wakitumia papai hupata nafuu na kupona haraka.
Pia papai husaidia kuleta nuru ya macho, kama inavyoaminika kwa karoti, hali kadhalika papai pia husaidia kupunguza madhara yatokanayo na moshi wa sigara.
Hivyo wavutaji wa sigara ni vyema wakatumia tunda hili mara kwa mara ili kujipunguzia madhara ya moshi wa sigara, ingawaje ni vyema wakakumbuka matumizi ya sigara si mazuri kwa afya hivyo ikibidi ni vizuri kuacha kabisa.
Ni wazi kuwa papai ni tunda lililosheheni kila aina ya utajiri wa vitamin kuliko matunda mengine, kwani lina vitamin A, B, C, D na E.
Wataalam wa tiba za asilia pia wanaeleza kwamba tunda hili linauwezo wa kutibu tatizo la usagaji wa chakula tumboni pia hutibu kisukari na pumu na mara nyingine hata kifua kikuu.
Tunda la papai lina faida nyingi sana kwa afya ya mwanadamu. Miongoni mwa faida hizo ni pamoja na kuwa na uwezo wa:
- Kutibu tatizo la Shida ya kusaga chakula tumboni
- Kutibu Udhaifu wa tumbo
- Kutibu Kisukari na asthma au pumu.
- Kutibu Kikohozi kitokacho mapafuni
- Kutibu Kifua kikuu
- Tunda hili huleta afya nzuri ukitumia kila siku
- Maziwa yanayotoka katika jani lake huponya vidonda
- Vilevile yanasaidia kutibu sehemu palipoungua moto
- Kama hiyo haitoshi, maziwa yanayotoka katika jani la mpapai yanatibu kiungulia na Ugonjwa wa colon (njia ya haja kubwa ndani)
Pia yanasaidia kutofunga choo
Maganda ya tunda la papai yanasaidia kutibu tatizo la kuungua, vipele na saratani ya ngozi.
Mbegu zake zinatibu ini zikitafunwa 10 – 12 kwa siku 5.
Majani
yake yakaushie ndani, yanatibu pumu. Inapoanza kubana yachome majani
yaliyokaushwa kisha jifukize, kule kubanwa kutakisha.
Majani yake yanasaidia katika kutibu shinikizo la damu.
Papai
likimenywa na kupondwa linafaa Sana katika masuala ya urembo kwani
linaweza kutumika Kama vile unavyotumia lotion kulainisha uso.
Mbegu za papai zina uwezo wa kutibu homa. Meza mbegu za papai kiasi cha kijiko cha chakula mara 3 kwa ajili ya kutibu homa.
Mbegu
za papai zilizokaushwa ndani kisha zikasagwa kuwa unga zinatibu
malaria, tumia kijiko 1 cha chai changanya na uji, kunywa mara 3 kwa
siku 5 Mgonjwa wa kifua kikuu akila matunda haya kwa muda mrefu atapona
bila dawa nyingine.
Mizizi
yake ikipondwa na kulowekwa katika maji yaliyochemshwa, lita 2 na nusu
kwa dakika 15, yanatibu figo, bladder, yanazuia kutapika. Nusu kikombe
cha chai kutwa mara 3 kwa siku 5.
Tikiti maji
TIKITI
MAJI ni moja ya matunda yanayolimwa sana katika maeneo mbalimbali
nchini Tanzania tofauti na miaka iliyopita.
Hii inaashiria kwamba tunda
la tikiti maji linaliwa sana katika maeneo hayo kutokana na faida
inayopatikana kwenye tunda hilo.
Faida ya kutafuna mbegu za tikiti maji
Pamoja
na kuongezeka kuliwa kwa tunda la tikiti maji lakini wengi wa wateja
wanaokula tunda hilo huwa hawajui faida ya mbegu za tunda hilo.
Kutokana
hali hiyo wengi wanaokula tikiti maji wanatema mbegu hizo na huenda
wengi walikuwa na imani potofu inayokataza kula mbegu za tunda.
Hivyo
badala ya kuzitafuna mbegu hizo wengi huzitema na kuona ni kitu kisicho
na faida yoyote katika mwili wa binadamu.
Lakini
mbegu hizo zinatakiwa kutafunwa wakati unapokula tunda lenyewe na hii
ni kutokana na faida zake kiafya.
Unapokula tunda la tikiti maji
unachotakiwa kufanya ni kuzitoa mbegu zake na kuziweka kwenye chombo
kimoja mpaka zichipue yaani kuanza kutoa mizizi.
Baada
ya hapo unatakiwa uzikaushe tayari kwa kuzitumia kutoka na faida hizi
zifuatazo:
Mbegu za tikiti maji zina protini nyingi hivyo kuzitafuna
kunaweza kumpatia mlaji chanzo cha protini.
Pia aunzi mmoja tu (takriban
ujazo wa 1/8 wa kikombe) inakupa virubutisho vya protini vya gramu 10.
Hii
ni sawa sawa na kiwango kinachopatikana kutoka katika yogati ya
Kigiriki wakati wa kustaftahi.
Mbegu ‘zilizochipua’ zimemea na mara
nyingi zina virutubisho vya hali ya juu kuliko zile ambazo
hazichipua.
Kuchipua kunaondoa mchanganyiko katika chakula ambacho
husababisha ugumu wa kufyonza virutubisho vyote.
Mbegu
za tikiti maji zilizochipua zikitafunwa huongeza msongamano wa
virutubisho na kusababisha urahisi kumeng’enya chakula.
Kuhusu
tikitimaji, mbegu hutolewa ngozi nyeusi ya juu na kubaki ikifanana na
mbegu zilivyo.
Katika mbegu za zamani hili halipatikana lakini
umegundulika kwamba kweli mbegu hizi zinaleta afya kwenye mlo.
Mbegu
za tikiti maji zilizochepua zina protini, vitamin B, Magnesia, na
mafuta ambayo hayakoleza.
Wataalamu wa masuala ya chakula wanasema
mafuta yaliyokolezwa mara nyingi hayana viwango vya lehemu na muasho na
yanaondoa hatari ya kupata ugonjwa wa moyo na kiharusi.
Kama
umeshawahi kutafuna mbegu za matikiti maji wakati ukila tunda hilo
uligundua ladha yake ni sawa na tunda lenyewe.
Mbegu za matikiti maji
ni sawa na mbegu za alizeti kwa ladha, lakini haina lozi kubwa.
Zinakuwa
na ladha nzuri zaidi zikiwa kwenye kachumbari, iliyochanganywa pamoja
au ukiila ikiwa mkononi mwako.
Jungu na mbegu nyingi ni nzuri kwa mwili
wa mwanadamu, lakini ukilinganisha ukubwa wa lishe unaopatikana basi
mbegu za matikiti maji
Kama vile haitoshi tunda hili limejaaliwa virutubisho kadha wa kadha vyenye faida kubwa katika afya ya mwanadamu.
Licha
ya 92% ya tikiti maji kuwa ni maji, bado zile 8% zilizobaki zina faida
kubwa sana kiafya jambo linaloonekana kutofahamika kwa wengi. Zifuatazo
ni baadhi tu ya faida chache kati ya nyingi za tunda hili la tikiti
maji:
Tikiti
maji ni chanzo kizuri cha vitamini. Katika tunda hilo kuna Vitamin A,
inayosaidia kuboresha afya ya macho na pia kuondosha sumu mwilini;
Vitamin C, inayosaidia kuboresha kinga, kuponya majeraha, kukinga
uharifu wa seli, kuboresha afya meno na fizi; na vitamini B6,
inayosaidia ubongo kufanya kazi na pia kuibadilisha protini kuwa
nishati.
No comments:
Post a Comment