Kwa
ujumla tangawiz hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500 kutoka
usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na tangawiz
zinastawi.
KUANDAA SHAMBA
Andaa
Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya April, may au June, ni
vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa miaka mitatu,
Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia November
unaweza kuanza kupanda.
.
KUPANDA
Tangawizi
hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake. Panda
tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60 kati
ya mstari mmoja na mwingine. Tumia mbolea ya mboji au samadi na
usitumie mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa
katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea
ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz. Huchukua wiki
mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na
joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na
kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili
ya kwenda kupanda. Palilia Mara Majani yanaoota na pandishia udongo
kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.
MAGONJWA
Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).
KUVUNA
Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
Tangawiz
haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji yakituama
kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz huwa ya njano
na huanza kunyauka
Kuvuna
Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko
linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja,
kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport,
wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani
Uzuri tangawiz unaweza kusubir soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka
Jamani tusiogope kuwekeza, na kujaribu fursa mpya, Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali
Watu
wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa kukosa mitaji ya
kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua
kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzĂ lisha mbegu ambazo
utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata
uzoefu kupitia hapo na kujua kama eneo ulilolima ni sahihi na linafaa
kwa kilimo cha tangawiz.
Sokoni
tangawiz huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri, pia
tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg. Usikatishe tamaa
pale tangwiz inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubir kwa mda mfupi
na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa hupanda kwa
haraka
HALI YA HEWA
Mimea
hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali
ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji,
magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti hukua vizuri katika
maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo
mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za
sentigrade huchelewa kuota
Mvua: kwa
upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita
400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi
na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji
udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji
udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya
udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una
uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0.
No comments:
Post a Comment