Kwa
kawaida makundi ya nyuki katika nchi ya Tanzania na baadhi ya nchi
zinazolingana kwa tabia za nchi, makundi ya nyuki huanza kutafuta sehemu
salama na yenye chakula kwa wingi kuanzia mwezi wa kumi katika mwaka
mpaka mwezi wa nne kwa mwaka unaofuata.Kipindi hiki huwa na makundi
mengi yanayozunguka hapa na pale kutafuta nyumba ambayo itawafaa kwa
ajili ya makazi yao na kwa ajili ya kuhifadhia chakula.
Hiki
ndio huwa kipindi muafaka sana kwa wafugaji kuanza kutega mizinga
ambayo imeshaandaliwa kwa ajili ya kufugia nyuki.Kwa kuwa makundi mengi
huwa yanatafuta sehemu za makazi hivyo ni rahisi sana kuyakama na
kuyahifadhi makundi hayo kwa ajili ya uzalishaji wa mazao ya nyuki.
Kutokana
na hilo, mfugaji anapaswa kuanza kuandaa sehemu ya kufugiua nyuki na
mizinga yake mapema zaidi kabla ya msimu huo kufika ili asiweze kukosa
makundi ya nyuki.Unashauriwa kuanza kuandaa mazingira ya kufugia nyuki
na mizinga angalau mwezi mmoja kabla kwa kusafisha, kukarabati au
kutengeneza kile unachokihitaji.
VIFAA VINAVYOPASWA KUANDALIWA.
Kabla
ya kuanza kufuga nyuki kuna vifaa ambavyo mfugaji wanyukiu anapaswa
kuanza kuviandaa mapema kabla ya msimu wa ufugaji wa nyuki kufika.Vifaa
hivyo ni kama vifuatavyo:-
UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Eneo
ambalo kuna wanyama wa aina mbalimbali ambao wanaweza kufanya uharibifu
mbalimbali wa mizinga pindi ikiwa na nyuki na kusababisha uharibifu wa
mizinga, kuua nyuki au hata mnyama mwenyewe kufa kutokana na kudungwa na
nyuki.Hivyo ujenzi wa mabanda ya kufugia nyuki ni vyema ukafanyika.
DHAMIRA YA UJENZI WA MABANDA YA KUFUGIA NYUKI.
Mabanda hayo ya kufugia nyuki yanaweza kuwa ya udongo, tofali au ya miti pekee pande zote, milango pamoja na kuezekwa kwa nyasi.
Kuna sababu mbalimbali ambazo zinasababisha mfugaji nyuki kuweza kujenga mabanda ya kufugia nyuki, miongoni mwa sababu hizo ni:-
1. Kukinga mizinga na jua na mvua.
Hii
ni sababu moja wapo ambayo inasababisha mfugaji wa nyuki kuamua kujenga
mabanda ya kufugia nyuki, mzinga unapokuwa kwenye kivuli huusaidia
mzinga kuweza kudumu kwa kipindi kirefu, pia kivuli husaidia nyuki
kufanya kazi zao kwa juhudi.Iwapo mzinga utakuwa upo kwenye jua nyuki
hutumia muda mwingi kupunguza joto la ndani ya mzinga badala kutumia
muda huo kwa ajili ya kutafuta chakula.
Nyuki
wanapoona jua ni kali zaidi na kusababisha joto kali ndani ya mzinga
huamua kuhama katika mzinga huo na kwenda kutafuta makazi sehemu
nyingine.Hivyo nio vyema mzinga ukakaa kwenye kivuli na sehemu isiyoweza
kunyeshewa na mvua.
Pia
mvua inaponyeshea mzinga husababisha mbao kuweza kuoza ndani ya muda
mfupi, hivyo kwa kujengea banda la kufugia nyuki huweza kuukinga mzinga
wako dhidi ya mvua ambayo inasababisha kuozesha mbao za mzinga wako.
2. Kukinga na wanyama waharibifu
Mabanda
haya ya kufugia nyuki husaidia sana kwa wanyama waharibifu wa mizinga
kushindwa kuifikia mizinga lakini pia husaidia sana kupunguza
mashambulizi ya nyuki kwa viumbe wengine.Mizinga huwekwa ndani ya banda
na banda kufungwa milango.
3. Ulinzi na ukaguaji
Ujenzi
wa mabanda ya kufugia nyuki husaidia sana kuiweka mizinga yako sehemu
salama dhidi ya wezi wa mizinga au asali lakini pia husaidia sana wakati
wa uangalizi wa mzinga.Mizinga inapokuwa pamoja uangalizi wa mizinga
hiyo huwa ni rahisi sana na pia huweza kusaidia kipindi cha uvunaji na
uwekaji wa kumbukumbu za kila mara.
Pembeni
ya banda hilo sehemu ambazo mizinga inawekwa huwekwa matundu maalumu ya
kutoka na kuingia nyuki kwa ajili ya kujitafutia chakula chao.
MIZINGA YA KUFUGIA NYUKI.
Mizinga
ya kufugia nyuki inapaswa kuandaliwa mapema kabla ya msimu wa kukamata
makundi ya nyuki haujafika.Mizinga inayopaswa kuandaliwa ni kama
ifuatayo:-
1. Mzinga wa kibiashara
Huu
ni mzinga wa kisasa unaotumika kwa wafugaji wa nyuki hasa wale
wanaotaka kuvuna asali kwa wingi kwa ajili ya kuuza.Mzinga huu huweza
kuzalisha asali kwa wingi kadri misimu ya uvunaji inavyoongezeka mwaka
hadi mwaka.
Mzinga huu una sehemu kuu tatu kama zifuatazo:-
A. Box la kuzalishia watoto wa nyuki
Ni
box ambalo kwa kawaida huwa la kwanza kwa upande wa chini.box hili
ndilo ambalo huwa na mlandfo wa nyuki kuingia na kutoka pindi
wanapokwenda na kutoka kwenye utafutaji wa chakula.Box hili hutumika na
malikia wa nyuki kwa kutagia mayai pamoja na kulelea watoto ambao
husubiri kuanguliwa na kuwa nyuki kamili.
Pia
box hili hutumika kwa ajili ya nyuki kuhifadhia chakula chao kwa ajili
ya msimu wa kiangazi, msimu ambao huwa hauna maua yenye chakula cha
nyuki cha kutosha,Hivyo mfugaji hapaswi kuvuna asali anayoikuta katika
brood box, kwa kuvuna asali unayoikuta katika brood box husababisha
kundi lako kuhama kwa kukosa chakula.
Kwa
kawaida matumizi ya mzinga huu huanza kuvuna asali baada ya wastani wa
misimu miwili mikubwa yaani sawa na miaka miwili.Na mara baada ya
kipindi hicho kipita mfugaji huweza kuanza kuvuna kwa vipindi tofauti
tofauti vya mwaka na kuendelea.
B. Kitenga malikia
Hiki
ni kifaa kama nyavu ambacho huwekwa kati ya brood box na super box,
wavu huu huweza kumzuia malikia asiweze kupanda katika super box kwa
lengo la kutaga mayai.matundu ya waya huu ni madogo kulingana na umbile
la nyuki watenda kazi peke yao.Hivyo malikia na madume ya nyuki hayawezi
kupanda kuelekea kwenye super box.
C. Box la kuhifadhia asali
Hili
ni box ambalo huwekwa juu mara tu baada ya queen excluder.Box hili huwa
ni maalumu kwa nyuki watenda kazi kuweza kuhifadhi asali yao kwa
wingi.Asali inayokuwa katika box hili haiwezi kuchanganyika na watoto wa
nyuki wala chavua kutokana na kuwapo kwa queen excluder chini
yake.Asali inayotoka katika Box hili huwa nzuri na safi kutokana na
kutochanganyika na masega ambayo yalitumika kwa kuangulia watoto wa
nyuki.
Uvinaji
wa asali katika mzinga huu, mfugaji anapaswa kutoa frame zilizopo
katika super box ambazo asali yake tayari imeiva.Mara baada ya kutoa
frame hizo mfugaji anapaswa kukamua asali hiyo kwa kutumia mashine ya
kisasa iitwayo Honey Centrifuge Machine.Mashine hii huweza kufyonza
asali yote iliyopo katika sega na kubakiza sega likiwa halina asali.
Mara
baada ya hapo mfugaji anapaswa kurudisha sega hilo kwenye mzinga likiwa
na frame yake ili nyuki aweze kujaza asali tena.Hii inamsaidia sana
nyuki kumpunguzia kazi ya kujenga sega jipya la Sali kila baada ya mvuno
wa asali na hivyo kuongeza uzalishaji wa asali mara dufu.Tofauti tu ya
aina ya mzinga huu ni kwamba huwezi kupata zao la nta.
2. Mzinga wa viunzi
Huu
ni mzinga wa teknolojia ya kati kutoka kwenye mizinga ya kienyeji na
kuelekea mizinga ya kisasa.Mzinga huu uhifadhi wake wa asali
hautofautiani sana na uhifadhi wa asali katika mizinga ya kienyeji,
isipokuwa katika mzinga huu masega hupangwa kwa kufuata utaratibu wa
viunzi vilivyowekwa.nyuki huweka sega moja katika kila kiunzi kimoja cha
mzinga huu.
Mzinga
huu pia haujagawanywa kwa kutenganisha sehemu za kuhifadhia asali na
sehemu ya malikia kuangulia watoto.Hivyo asali itokayo katika mzinga huu
huweza kuchanyanyika na watoto iwapo mfugaji hatakuwa makini katika
uvunaji wa asali hiyo.
Uvunaji
wa mzinga huu, mfugaji anapaswa kukata sega lote lenye asali pekee na
kulihifadhi katika chombo kisafi kwa jili ya kukamua asali hiyo kwa
kutumia mashine ya kusasa au kwa kutumia njia za kitamaduni.
Aksante kwa somo zuri.
ReplyDelete