Sunday, May 21, 2017

Fahamu Kilimo Bora Cha Mdalasini - Cinnamon

 AINA
Mchanganyiko; za kienyeji (ndogo) na za kigeni ( kubwa)

HALI YA HEWA NA UDONGO

  • Mvua nyingi za kutosha 2000mm -2500mm kwa mwaka
  • Udongo wenye rutuba
  • Joto kwa wingi
  • Hewa yenye unyevunyevu


KUSIA MBEGU KWENYE VITALU

  • Mbegu hupatikana kwenye miti iliyokomaa
  • Sia mbegu kwenye kitalu zikiwa nusu sentimeta chini ya udongo
  • Baada ya kuchipua, mbegu huchukua miezi 6 hadi mwaka mmoja kufikia umri wa kupandikiza shambani
  • Panda miche wakati wa masika
  • Panda kwa nafasi ya 2m x2m. Nafasi hizi huwezesha miti kutoa machipukizi mengi. Nafasi kubwa hufanya miti kuwa na matawi mengi pia mashina hayanenepi wala kurefuka

 UTUNZAJI

  • Acha machipukizi kwenye shina
  • Toa matawi kwenye mashina ili kunenepesha mashina
  • Weka shamba katika hali ya safi
  • Zuia magonjwa kama.
  • Vinundu (galls)wanaosababishwa na utitiri na wadudu scales na mealbugs kwa kutumia dawa za sumu kama Selecron, Karate nk.


KUVUNA

  • Anza kuvuna miaka 3 baada ya kupanda
  • Mazao ya mdalasini ni maganda ya mashina ya miti
  • Kata shina la mti,na tenganisha maganda na mti kwa njia ya kumenya
  • Kuwa mwangalifu ili ganda litoke vizuri bila kupasukapasuka
  • Seli za nje ya ganda la mdalasini ni chungu hivyo ni vizuri ziondolewe kwa kukaruza kwa kisu
  • Kausha vizuri siyo kwenye jua kali Mavuno
  • 0.25 kg – 10kg maganda yaliyokaushwa kwa mti mmoja. Kiasi cha mazao hutegemea ukubwa na umri wa mti
  • Ubora wa mdalasini hushuka kulingana na umri wa mti. Mti wa umri mkubwa hutoa mganda yenye ubora wa chini

 MATUMIZI

  • Mdalasini baada ya kukaushwa ikiwa umesagwa au bila kusagwa hutumika kama:
  • Kiungo kwenye chakula na vitafunwa kama keki, mandazi,vitumbua
  • Vikolezo kwenye vinjwaji km. chai, kahawa
  • Dawa ya tumbo hasa wakati wa kuvimbiwa, kutoa hewa tumboni pia kuongeza hamu ya chakula
  • Dawa ya ngozi


JINSI YA KUTUMIA

  • kiungo kwenye chakula
  • Tumia maganda au saga magada yaliyokauka. Tumia ili kuongeza ladha kwenye vyakula kama pilau, ndizi, mchuzi nk 
  • Kutengenezea kinywaji
  • Weka vipanda vichache 2-3 (30gm) vya maganda kwenye kikombe ongeza maji yanayochemka, funika kwa dakika 15, ongeza vipande vya limao. Kunywa kila baada ya kula

MANUFAA

  • Miti hudumu shambani zaidi ya miaka 20. Miti huchipua na kutoa machipukizi mengine kila baada ya kuvuna
  • Gharama ndogo ya uzalishaji
  • Mazao yaweza kuhifadhiwa kwa muda mrefu
  • Magonjwa na wadudu ni kidogo
  • Rahisi kuchanganya na mazao mengine
  • Nguvu kidogo, kipato kikubwa.

No comments:

Post a Comment