UTANGULIZI
kwa hapa Tanzania korosho ulimwa na kustawi vizuri katika mikoa ya kusini Mtwara, lindi, na maeneo kama Mafia, bagamoyo na Rufiji.
mvua; korosho ustawi vizuri kwenye maeneo yenye mvua 840mm - 1250 mm wastani wa mvua kwa mwaka,
napia hukua vizuri kwenye maeneo 0- 500 m kutoka usawa wa bahari.
udongo; korosho ukua vizuri kwenye maeneo yenye PH 5.6 udongo wa kichanga (sandy) na pia udongo mfinyazi kichanga.
KUANDAA SHAMBA
kama mazao mengine shamba la korosho linatakiwa kusafishwa, kusawazishwa nakutifuliwa vizuri kwaajili ya kupanda korosho.
nakatika mashimo utakayo chimba unaweza kuweka mbolea ya ngombe ukachanganya na udongo mapema ili kuongeza rutuba.
KUPANDA
Ni muhimu sana kuchagua mbegu bora kwa kua mbegu utakayo panda ndo itakuonesha kiasi gani utavuna,
- baada ya kununua mbegu unachukua maji na chumvi 100g ya chumvi unaweka katika maji kiasi cha lita 5 unakoroga vizuri na unachukua mbegu zako unaweka kwenye maji hayo zile zitakazo zama ndio mbegu zenye uwezekano mkubwa wa kiota,
napia unashauriwa kuto panda mbegu zenye umri zaidi ya mwaka mmoja,
nafasi ya kupanda 12m x 6m kwenye maeneo mvua na kiasi cha miti kitakua 139/hectare
kwenye maeneo yasio na mvua za kutosha ni 12m x 12m na kiasi cha miti ni 69/ hectare
MUHIMU
Kuna aina mbili ya kupanda mbegu ya korosho
- kupanda moja kwa moja; hii ni njia mambayo ni risk sana na inaitaji umakini kwa sababu kunauweze3kano mkubwa wa mbegu kufa. ukitumia njia hii unatakiwa kupanda mbegu tatu 3 katika shimo moja na baada ya miezi mi 3 - 4 ngoa mimea na bakiza mmoja wenye afya na muonekano mzuri.
- njia ya kitaru; hii ni njia ya pili na ni nzuri kwa sababu unakua huru kuchagua mche ambao umestawi na ulio na muonnekano mzuri , unatakiwa kuamishia miche shambani ikiwa na umri wa wiki 6 na zingatia kuchagua mche wenye afya.
MAGONJWA NA WADUDU
MAGONJWA
- Anthracnose
- powdery mildew
WADUDU
- Cashew stem girdler
- cashew weevil
- coconut bug
- heliotropes bug
- meal bug
- trips aphids
ili kuzuia maagonjwa na wadudu unatakiwa
- palilia mapema
- weka shamba katika hali ya usafi
- tumia mbinu ya kuchanganya mazao kwa korosho unaweza kuchanya pamba au maharage hiyo inasaidia kukimbiza wadudu wengine ambao wanakua hawapatani na mazao hayo
- tumia pesticide kutibu magonjwa
- tumia insecticide kuuwa wadudu waalibifu.
Korosho ufikia hatua ya kuzaa matunda pale inapo kua na umri wa miaka 2 1/2 hadi miaka mitatu
napia matunda ukomaa pale inapo kua na miaka 9 hadi 10
uwezekano wa mkoroso kuishi ni miaka 30 hadi 40
na kuvuna hua kunaanza mwezi october hadi mwezi december
MATUMIZI
- chakula
- hutumika kutengeneza rangi
- kama zao la biashara
- miti yake hutumkia kama kuni
- kutengeneza dawa e.t.c
za kazi ndugu, nahitaji kujua ni sehemu gani katika mkoa wa singida inafaa kwa kilimo cha korosho?
ReplyDelete