Wednesday, May 24, 2017

KILIMO CHA MAHINDI

KILIMO CHA MAHINDI (Maize)
    Mahind ni chakula bora na tegemezi kwa jamii ya africa. Takribani asimia 65 ya watu wengi wanatumia zao hili kwa chakula na kwa biashara pia.Mahindi yan virutubisho kama vile Protin,Wanga,Vitamin B, Madini chuma na mengineyo ambayo ni muhimu katika kujenga mwili. seehem nying mahind yanaliwa kwa njia tofauti tofaut kwa mfano mahindi mabichi kwa kuchomwa, kuchemshwa, kukaangwa na makavu hukobolewa na kusagwa ambapo hutumika kama lishe.
  
KUANDAA SHAMBA
      Kabla ya kupanda mahindi unatakiwa kuandaa shamba kabla ya mvua za kwanza za msimu. Shamba linatakiwa kuandaliwa kwa kutifuliwa vizur kwa vifaa vifuatavyo
  •        Trekta
  •         plau
  •         jembe la mkono
UPANDAJI WA MAHIND
1. Mbegu
    Upandaji wa mahindi unatakiwa pale tu mvua zinapoanza kunyesha. Kuchelewa kwa siku moja kupanda mahindi kunaweza kukusababishia kukosa mavuno mazuri kwa asilimia 1 hadi 2. Kupanda mahindi kwa mkono kwenye hecta moja huhitaji siku tano hadi nane ili kupanda kwa uhakika. Mbegu inatakiwa kupandwa kwenye shimo lenye urefu wa sentmita nne hadi tano ili kuzuia mbegu kuchepua kwa mvua zisizo na uhakika na pia kuzuia kuungua jua pindi hazijachipua na mvua hazinyesha vizuri
    Ekari moja hupandwa mifuko 4 hadi 5 yenye ujazo wa kilo mbili na pia kwa hecter moja tunapanda kilo 25 za mbegu.
  Ili kupata mahindi mazuri yaliyonyooka ni vyema kutumia mbegu bora za kisasa na za muda mfupi kama vile PANNER, TMV1, TMV2, STUKA na n.k mfano wa mahindi yaliyopandwa kitaalam


       

   





3. Mbolea
     mbolea husaidia kuweka mazao kukua haraka na kustawi vizur ili kuongeza uzalishaji wa mahindi kwa wingi. zipo aina mbili za mbolea ambazo ni
  •   mbolea za viwandani na 
  •   samadi
 mbolea za viwandani ni nzur huleta tofaut katika mahind kwa haraka lakini sio nzur kwa kurutubisha aridhi. mbolea hizi zin chumvichumvi hivyo husababisha kuua viumbe vya asili kwenye aridhi vinavyosaidia katika ukuaji wa mahindi
   Mbolea za samadi ni bora na ninzuri kutumia kwenye kilimo kwa sababu huongeza rutba kwenye mahindi na mimea mingine kwenye shamba kwa sababu haina kemikali zozote

4. Palizi
     kupalilia mahindi kunatakiwa ndani ya wiki 2 hadi3 baada ya kuota hii husaidia kutopoteza virutubisho muhimu ndani ya shamba ila mahindi yasiathiriwe na kupoteza ubora wake

5. Kukomaa na kuvuna
    mahindi yanatofautiana kukomaa na uvunaji wake kutokana nambegu iliyopandwa. kwa mbegu za muda mfupi huchukua siku 75 hadi 90 kukomaa haddi kuvunwa. Na mbegu za muda mrefu huchukua siku 95 hadi 125 kukomaa na kuvunwa pia.                                                                                                                                  Ni bora kutumia mbegu za muda mfupi ili kupata mavuno mazur na kwaq muda mfupi sababu unapopanda mbegu za muda mrefu mvua zinaweza kukata njiani hivyo kusababisha mahindi kuto beba vizur 


        Natumaini umejifunza kitu kupitia makala hii.

No comments:

Post a Comment