Kwa ujumla tangawiz hustawi kwenye mwinuko kuanzia m 800 mpaka 1500
kutoka usawa wa bahari, kwa ujumla maeneo mengi inakostawi kahawa na
tangawiz zinastawi.
KUANDAA SHAMBA
Andaa Shamba lako mapema, katua/lima kuanzia miezi ya April, may au
June, ni vizuri ukaanzisha Shamba jipya au lilikaa bila kulimwa kwa
miaka mitatu, Lainisha udongo miezi ya August au September na kuanzia
November unaweza kuanza kupanda.
.
KUPANDA
Tangawizi hupandwa kwa kuivunja vunja kwa kufuatisha mbingili zake.
Panda tangawiz kwa cm 30 kati ya shina moja na jingine na cm 45 mpaka 60
kati ya mstari mmoja na mwingine. Tumia mbolea ya mboji au samadi na
usitumie mbolea za kemikali kupandia, Kg 1000 za tangawiz hupandwa
katika hekta moja na unaweza kuvuna kuanzia tani 10 mpaka 25 inategemea
ukubwa wa mbegu, urutubishaji, kiasi cha maji na paliz. Huchukua wiki
mbili mpaka mwezi mmoja na nusu tngwz Kuota inategemea kiasi cha maji na
joto kwenye udongo, ni vizuri kuzitandaza tangawz kwenye kivuli na
kufunika na gunia na kuzimwagilia ili ziote kabla hujazikataka kwa ajili
ya kwenda kupanda. Palilia Mara Majani yanaoota na pandishia udongo
kwenye mashina ili tangawiz itanuke vizuri.
MAGONJWA
Tangawiz haishambuliw sana na magonjwa ila Mara chache hushambuliwa na kuvu (fungus).
KUVUNA
Huchukua miez 6 mpaka 18 mpaka kukomaa inategemea mwinuko toka usawa wa bahar na mvua.
Tangawiz haitaki maji yanayotuama kama vijaruba vya mpunga, maji
yakituama kwenye shina la tangawiz kwa mda Fulani Majani ya tangawiz
huwa ya njano na huanza kunyauka
Kuvuna Tani 10 kwa hekta moja ni kadirio la chini kabisa.. Kipindi soko
linapokua zuri unaweza kupata kuanzia Mil 20 mpaka 60 kwa hekta moja,
kuna wahindi ambao hununua tangawiz kwa wingi sana na wanaexport,
wahindi hununua kg 1 kwa sh 3000, mpaka 3500 ukiuzia shambani
Uzuri tangawiz unaweza kusubir soko zuri na ukauza kwa bei nzuri kwani zao hili hupanda bei haraka
Jamani tusiogope kuwekeza, na kujaribu fursa mpya, Nina imani nimeeleweka na karibuni kama kuna maswali
Watu wengi wanashindwa kuzalisha tangawiz kwa wingi kwa kukosa mitaji ya
kununulia mbegu kwani mbegu zake ni gharama, hivyo unashauriwa kununua
kg chache walau kg 200 ukapanda eneo Dogo ili kuzĂ lisha mbegu ambazo
utaweza kuzisambaza eneo kubwa, na kwa kulima eneo Dogo unaweza kupata
uzoefu kupitia hapo na kujua kama eneo ulilolima ni sahihi na linafaa
kwa kilimo cha tangawiz.
Sokoni tangawiz huuzwa sh 5000 mpaka 6000 kwa kg soko linapokua zuri,
pia tangawz kuna msimu hushuka bei mpaka sh 2000 kwa kg. Usikatishe
tamaa pale tangwiz inashuka bei mpaka sh. 1500, unaweza kusubir kwa mda
mfupi na kuuza tangawiz kwa bei nzuri sana kwa kua bei yake huwa
hupanda kwa haraka
HALI YA HEWA
Mimea hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili
hali ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha
maji, magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti hukua vizuri
katika maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi.
Iwapo mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za
sentigrade huchelewa kuota
Mvua: kwa
upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya millimita
400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa ya fungusi
na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile
haihitaji udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa.
Hali ya udongo katika kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea
una uwezo vile vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
Sasa mbona unachanganya maada? Unaelezea kuhusu tangawizi huku mwishoni unaongelea matikiti!
ReplyDeleteThis comment has been removed by the author.
ReplyDeleteShukrani sana kwa elimu ya tangawizi napenda kujua pia juu ya wahindi wanaoexport wanapatikanaje nisaidie kujua maananina heka2 na zipo tayari
ReplyDelete