Tuesday, May 30, 2017

KWA KILIMO CHA MAHINDI YA KUCHOMA (GOBO)


Kuna hii biashara ya mahindi ya kuchoma (maarufu kama gobo). Unaweza kulima kwa kutumia mtaji kidogo na kupata sarafu za kutosha. Angalia mchanganuo ufuatao: kukodi shamba ekari moja wastani wa tsh 50,000/=, kulima 30,000/=, kupalilia 30,000/=, mbolea mifuko mi-3, tsh 150,000/=, madawa wastani tsh 50,000/=; Jumla kuu ni tsh. 310,000/=. Gharama hii hauitoi mara moja bali ni kidogo kidogo kutegemea
hatua husika. Mahindi huchukua wastani wa siku 90 (miezi mitatu) tangu kupanda hadi kugoboa (yaani kuvuna haya mahindi mabichi).
Unaweza kupanda kwa kutumia mvua au kutumia umwagiliaji mahali popote Tanzania. Kwa ekari moja ukilima kwa kuzingatia utaalamu una uhakika wa kuvuna kuanzia mahindi 9,800. Hindi moja huuzwa kwa tsh. 150/= hadi 250/=, kutegemea hali ya soko kwa bei ya jumla. Ukikokotoa utaona kuwa kwa ekari moja unaweza kupata tsh. 1,470,000/= kwa kadirio la chini na tsh. 2,450,000/= kwa kadirio la juu.
Ukitoa gharama za uendeshaji (za moja kwa moja) unaweza kukunja faida ya hadi tsh 2,140,000/= kwa kadirio la juu. Ukilima eka 5, una uhakika wa faida ya tsh milioni 10.7. Je, ukilima misimu kadhaa, bado utashindwa kujenga nyumba ya maana au kuwa na maisha yenye unafuu? Bila shaka utaweza! Unachohitaji wewe ni mambo yafuatayo: utayari, uthubutu, kuwa-up-to-date kwa taarifa za misimu na masoko na uwe ni mtu wa kufuatilia fursa na kujifunza. Fursa zipo 'bwerere', kama una 'allergy' na kilimo tafuta na ujifunze fursa nyinginezo; LAKINI; mtu YEYOTE anaposema fedha ni ngumu, kiukweli anakuwa hayupo "serious" kabisa na haya maisha!
MAISHA NI VITA!

29 comments:

  1. Kwa makadirio ambayo umeonyesha, mahindi 9,800, umetumia spacing kiasi gani kati ya hindi na hindi na kati ya mstari na mstari?
    Je kuna mbegu ambayo ina zaa mahindi mawili ambayo ni ya size mija kwa ukubwa. Kwa ukanda wa pwani bagamoyo. Ni mbegu gani inayo fanya vuzuri?
    Wazo hili linawezekana lisiwe sahihi kama litahusisha uwekezaji wa mfumo wa umwagiliaji. Gharama za umwagiliaji zipo juu sana. Unaweza ku share nami uzoefu weni kwenywe umwagiliaji wa zao hili.

    ReplyDelete
  2. Hiki ni kilimo bora sana sema hali ya soko ndio shida kwa kweli

    ReplyDelete
  3. Kiwango cha mahindi 980,000 kwa mimi mtalaam ni nusu heka tu kwa heka zote eiza za kiasili au kisasa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kweli fursa za kumwaga ila sisi hatuzion

      Delete
    2. Ndugu habari! Najua sijachelewa, tushirikiane kuufukuza umasikini, nipe mbinu.0768041537

      Delete
  4. Always tunatumia spacing ya (75 × 30)cm² ,kwa ekari za asili NI sawa na Miche 21,000 ya mahindi na standard eka ambazo ni ndogo kuliko za kienyez NI wastan wa Miche 17,000 ya mahindi

    ReplyDelete
  5. Hakika hiki ni kilimo bora na chenye tija kwa vijana, swali langu ni ipi mbegu nzuri kwa nyanda za juu kama Iringa

    ReplyDelete
  6. Kwa kweli hiki ni kilimo bora sana najuata nilikuwa wap siku zote na nikizuri sana kwa watu wa moshikilimanjaro asante sana.

    ReplyDelete
  7. Kuna aina mahindi ya kuchoma ambayo yakikomaa yanaoza yanaitwaje?

    ReplyDelete
  8. Kwakweli nimeipenda sana,mimi nikija nahitaji kufanya kilimo hiki nahitaji msaada wenu wazoefu nipo songea

    ReplyDelete
  9. Utafiti wako haupishani na ukweli. Ipo tofauti kidogo sana. Hapa Dar nimemaliza kuuza mahindi yangu leo, kwa hela 1 ukiondoa gharama za matunzo ya shamba nimepata m2.

    Muhindi 1 nmeuza kwa sh 300 na 250 kwa mahindi madogo

    ReplyDelete
  10. Vingine tunaumiza kichwa bure tu kumbe mambo ni simple

    ReplyDelete
  11. Mahindi mabichi wapo wateja wauwakika

    ReplyDelete
  12. Nmepanda mahindi yakutosha eka 5 kama kuna tajiri anaweza nunua nitumie namba zao

    ReplyDelete
  13. Mbegu gani zinafaa kwa ukanda wa Pwani???

    ReplyDelete
  14. Hakika wengi hiki kilimo wanakipuzia lakini ni kilimo ambacho kinaweza kumtoa mkulima kwa haraka saan endapo utafata njia sahih

    ReplyDelete
  15. Kilimo bora Sana binafsi nauza mahindi ya kuchoma 1 kwa tsh. 500

    ReplyDelete
  16. Sanahani naona hesabu zako hazijakaa vizuri, kwa vipimo ulivyosema 75cm x 30cm ni kweli unapata miche Elfu 21+ nilitegemea uniambie utapata mahindi kuanzia 30,000 kwa sababu ninategemea nusu ya mahindi yatazaa mawili mawili.

    ReplyDelete
  17. Amina,, tushindwe sie maana sisi ni wazee wa hakuna ajira.. Hongera sana bro na asante kwa ushauri

    ReplyDelete
  18. Twende watanzania kazi iendelee

    ReplyDelete
  19. Naomba kuuliza mbegu zipi zinafaa ukanda wa mtwara hususani tandahimba? Ya kuchoma na hukomaa kwa muda mfupi?

    ReplyDelete