Sunday, May 28, 2017

UFUGAJI WA NGURUWE.

UFUGAJI WA NGURUWE
Nguruwe ni mnyama asiecheua na mwenye kwato zilizogawanyika.
AINA ZA NGURUWE (BREED)
i) Largewhite
-Rangi nyeupe
-Masikio yao yamesimama wima
-Wana miili mikubwa
-Ni wazazi wazuri
-Hutoa nyama nzuri
ii) Landrace
-Rangi nyeupe
-Masikio yao yamelalia mbele
-Mwili mrefu
-Wana nyama nzuri
-Ni wazazi wazuri
iii) Saddleback
-Rangi nyeupe na baka jeusi mgongoni au rangi nyeusi na baka jeupe mgongoni
-Wana masikio yaliyolala
-Ni wazazi wazuri
-Wanatoa nyama nzuri
FAIDA ZA NGURUWE KWA UJUMLA
-Hutoa nyama nyeupe ambayo ni nzuri sana kwa binadamu
-Ni rahisi kutunza kwani wana uwezo wa kula mabaki ya vyakula
-Huzaa kwa wingi na kwa muda mfupi
-Hutoa mbolea kwa ajili ya kilimo
-Hutoa mafuta kwa ajili ya kupikia n.k
AINA ZA UFUGAJI
-Ufugaji wa ndani
Nguruwe hufugiwa kwenye banda tu 100% bila kutoka nje
-Ufugaji wa nje
Nguruwe kufugiwa nje kwa muda mwingi 70%-80%
-Ufugaji wa ndani na nje
Nguruwe kufugiwa ndani ya banda na nje kwenye uzio/fence @50%.
MAMBO YA KUZINGATIA KATIKA UFUGAJI WA NGURUWE
-Upatikanaji wa soko kwa ajili ya mazao ya nguruwe
-Aina ya nguruwe unaotaka kufuga kulingana na lengo
-Mtaji kwa ajili ya kuendesha mradi
-Eneo zuri la kuwafugia
-Upatikanaji wa chakula cha kuwalisha
-Utaalamu
VYAKULA VYA NGURUWE NA ULISHAJI
Utunzaji na ulishaji wa nguruwe  umegawanyika katika makundi
-Nguruwe wadogo/watoto
-Nguruwe wanaokua
-Nguruwe wenye mimba
-Nguruwe mzazi au anaenyonyesha
-Nguruwe dume
VIINI LISHE VINAVYOTAKIWA KWENYE CHAKULA CHA NGURUWE
-Wanga (kuupa mwili nguvu)
Pumba za mahindi au mpunga
-Protini (kujenga mwili)
Mashudu aina zote na unga wa dagaa
-Madini
Chokaa, chumvi na pigmix/pigboost
-Vitamini
Majani au mbogamboga
-Maji ni muhimu sana kwa kila kiumbe hai
BAADHI YA MAGONJWA  YANAYOWAPATA NGURUWE NGURUWE
i) African Swine Fever (homa ya nguruwe)
Huu ni ugonjwa hatari sana kwa nguruwe unaosababishwa na virus
ii) Swine dysentery
Huu ni ugonjwa wa kuhara husababishwa na bacteria aitwae treponema hyodyseteriae
iii) Respiratory disease
Ugonjwa wa mapafu
iv) Sarcoptic mange
Ugonjwa wa ngozi husababishwa na mangemites
v) Calibasilosis
Kwa nguruwe wadogo husababishwa na E.coli bacteria
vi) Coccidiosis
Kwa nguruwe wadogo
vii) Erysipelas
Huu ni ugonjwa wa nguruwe unasababisha vidonda vyenye umbo la almasi kwenye ngozi (diamond shaped lesions)
NB: Minyoo ni miongoni mwa vitu vinavyosumbua sana ukuaji wa nguruwe hivyo inashauriwa kuwapa dawa ya minyoo kila baada ya miezi mi3.

No comments:

Post a Comment