Ndugu
zangu, juzi Ijumaa nilikuwa kwenye maongezi ya kawaida na Dada yangu,
mwalimu na mshauri wangu Dada SUBIRA, ambae ndiye mmiliki wa Blogu ya
WAVUTI. Tulikuwa kwenye maongezi ya kifamilia, kisha nikamshirikisha
harakati zangu za ufugaji wa samaki, akapata hamasa, akaniomba
niwashirikishe na Watanzania wenzangu kwa maandishi. Na mimi
nikakubaliana na ombi hilo.
Unaweza
kufanikiwa sana tu, unaweza kuwa billionaire ama milionea. Chunguza
marafiki zako na watu unaoshinda nao waliofanikiwa, jifunze kwao na
usipojifunza utaendelea kuwa mlalamikaji.Fursa ya ufugaji wa samaki,
kilimo cha miti, kilimo cha nyanya na vitunguu ishakudondokea, usijjite
myonyenge, ama maskini maana ‘victim mentality isn’t going to get you
anywhere’ GO BIG OR GO HOME.
Ninachokiamini
katika maisha yangu ni kwamba, kila mtanzania anayonafasi kubwa sana ya
kuendesha maisha yake ya kila siku bila tatizo endapo atajitambua na
kuugundua ukuu wa Mungu ndani yake. Mwanadamu yeyote anaetambua uthamani
wake na bahati aliyopewa na Mungu ya kuendelea kuishi na kuzaliwa
Tanzania hawezi kuishi maisha ya kubangaiza.
Ndugu
zangu, juzi Ijumaa nilikuwa kwenye maongezi ya kawaida na Dada yangu,
mwalimu na mshauri wangu Dada SUBIRA, ambae ndiye mmiliki wa Blogu ya
WAVUTI. Tulikuwa kwenye maongezi ya kifamilia, kisha nikamshirikisha
harakati zangu za ufugaji wa samaki, akapata hamasa, akaniomba
niwashirikishe na Watanzania wenzangu kwa maandishi. Na mimi
nikakubaliana na ombi hilo.
Unaweza
kufanikiwa sana tu, unaweza kuwa billionaire ama milionea. Chunguza
marafiki zako na watu unaoshinda nao waliofanikiwa, jifunze kwao na
usipojifunza utaendelea kuwa mlalamikaji.Fursa ya ufugaji wa samaki,
kilimo cha miti, kilimo cha nyanya na vitunguu ishakudondokea, usijjite
myonyenge, ama maskini maana ‘victim mentality isn’t going to get you
anywhere’ GO BIG OR GO HOME.
Ninachokiamini
katika maisha yangu ni kwamba, kila mtanzania anayonafasi kubwa sana ya
kuendesha maisha yake ya kila siku bila tatizo endapo atajitambua na
kuugundua ukuu wa Mungu ndani yake. Mwanadamu yeyote anaetambua uthamani
wake na bahati aliyopewa na Mungu ya kuendelea kuishi na kuzaliwa
Tanzania hawezi kuishi maisha ya kubangaiza.
Katika
Makala yangu ya wiki hii ningependa kuwashirikisha kitu kidogo sana
nacho ni UFUGAJI WA SAMAKI KATIKA MAZINGIRA YA KIJIJINI KWA MTAJI MDOGO
SANA… kipindi cha nyuma, nilikuwa nikiwaona watanzania wenzangu hasa
huku Iringa, wakijishughulisha na ufugaji wa samaki, ni miaka miwili
imepita sasa, lakini nilikuwa ‘bize’ na mambo yangu sikutaka kujifunza
Zaidi kuhusu fursa hii. Mwanzoni mwa mwezi wa nane (8) mwaka jana 2014
rafiki yangu Nicolaus Kulangwa, ambae huko nyuma alinifundisha kilimo
cha Matango,alinipigia simu akinitaka nikataembelee mradi wake wa kufuga
samaki. Nilienda kijini kalenga hapa Iringa. Nilichokiona nilianza
kukifanyia kazi hapohapo na siku ileile. Wakati rafiki yangu akiwa na
jumla ya mabwawa saba ya samaki aiana ya sato na pelege mimi ndio kwanza
nilijutia muda ambao niliambiwa kuhusu fursa ile halafu nikazembea
kuifanya.
Kama
tunavyofahamu, lengo la uajasirimali ni kupata faida ya unachokifanya
na kugusa jamii inayo mzunguka mjasirimali. Na kama ilivyo kwa mifugo
mingine yeyote ile, kabla ya kuanza kufuga kuna mambo muhimu yanayopaswa
kuzingatiwa ili ufugaji wako uweze kuwa tija iliyokusudiwa na hivyo
kufikia malengo ya mfugaji huyo. Lakini kutokana na mazingira ya ufugaji
wa huku Iringa hasa Kalenga, nitayataja mambo hayo kwa kifupi sana,
mambo haya huenda yakatofautiana kutoka eneo moja la nchi hadi jingine,
na kwa vile mimi sijasomea chuo cha ufugaji wa samaki, maelezo haya ni
yale niliyoyapata kwa uzoefu tu, siyo ya kufundishwa chuo, mapungufu
yatakayogundulika na ‘wasomi’ wataniandikia email ili nikawashirikishe
wenzangu.
Mambo hayo ni kama ifuatavyo:
ENEO AMA SEHEMU YA KUWAFUGIA SAMAKI. Inasisitizwa
kwamba, eneo hilo liwe na udongo mzuri ambao hautaruhusu maji kupotea
hovyo. Udongo wa mfinyanzi ni mzuri na iwapo eneo lako lina udongo wa
tifutifu ama udongo wake ni kichanga unashauriwa kujengea kwa simenti
ama kuweka ‘kapeti gumu’ lisilo ruhusu maji kupotea.
UPATIKANAJI WA MAJI, wote
tunafahamu kwamba samaki huiishi majini, maji ndiyo roho ya masaki,
samaki ni maji na maji ni samaki. Hivyo eneo la kufugia lazima liwe na
maji ya kutoshana salama kwa kipindi cha mwaka mzima. Vyanzo vya maji
kwa ajili ya ufugaji wa samaki ni kama chemichemi, mito, maziwa na maji
ya ardhini hasa visima Kwa maeneo ya huku Iringa, tunabahati ya kuwa na
mto Ruaha ambao maji yake yapo muda wote wa kipindi chote cha mwaka.
Inashauriwa kwamba eneo hilo liwe salama ili kuwalinda samaki na mfugaji
kwa ujumla.
BWAWA. Bwawa
la samaki linahitaji nafasi kubwa ya ardhi, yenye mwinuko pamoja na
eneo la samaki kukimbilia. Hii ni njia rahisi ya ufugaji endapo ardhi na
maji havina gharama kubwa. Eneo kubwa zaidi linaruhusu uzalishaji
usiohitaji nguvu ya ziada na wenye tija.
MBEGU AMA VIFARANGA, mfugaji
wa samaki anashauriwa kutembelea maeneo ambayo wafugaji wakubwa
wanazalisha vifaranga ili aweze kupata mbegu bora anayohitaji. Kwa
wananaoishi Iringa na maeneo ya jirani, wanaweza kupata mbegu kwa bwana
Nicolaus.
UTUNZAJI WA BWAWA NA USAFI. Ili
mfugaji aweze kunufaika na miradi ya kufuga samaki ni lazima uafanye
usafi wa kutosha ndani nan je ya bwawa lake. Hasa kwa kuondoa majani ili
kuepusha wadudu na viumbe wengine kama konokono,vyura, nyoka, na kenge
wasiweze kufanya makazi na hatimaye wakawadhuru samaki. Hivyo, kila
unapoona uchafu, safisha mara moja.
ULISHAJI.
Tofauti na mifugo mingine kama kuku, samaki hawahitaji kula chakula
kingi sana. Katika hatua za mwanzo ulishaji wake unaweza kuwa mara tatu
kwa wiki ama Zaidi.
AINA YA CHAKULA. Samaki
wanaweza kulishwa kwa kutumia pumba ya mahindi, mashudu ya pamba na
alizeti, soya, mabaki ya dagaa, Karanga zilizosagwa, unga wa mahindi,
mabaki ya chakula kama ugali nk.
Kuna
mambo mengi sana ya kuzingatia unapaanza kufuga samaki, mambo mengine
ni kama vile kuzingatia miiundo mbinu, wafanyakazi, kuzingatia masoko,
utaalamu nk.
CHANGAMOTO KATIKA SAMAKI ni
magonjwa kama vile magonjwa ya samaki yapo mengi yakiwa nayasababishwa
na vimelea vifuatavyo magonjwa yanayosababishwa na bakteria, magonjwa
yanayosababishwa na virusi magonjwa yanayosababishwa na minyoo, magonjwa
yanayosababishwa na protozoa. na magonjwa yanayotokana na lishe duni.
Chanagamoto nyingine ni kama vile, Tatizo mojawapo ni la kuvuja kwa kuta
za bwawa. Tatizo hili hutokea iwapo ujengaji wa bwawa haukufuata
maagizo na taratibu za ujengaji wa bwawa. Kuna ndege, kenge, fisi maji,
nyoka hutokea. Iwapo bwawa lipo mbali na makazi. Kudumaa kwa samaki
kutokana na kuwa wengi bwawani kupita idadi inayotakiwa.
UVUNAJI WA SAMAKI. Hujudi
za mfugaji ndio zinaweza kupelekea kuvuna samaki wa kutosha na kumletea
faida kwa muda mfupi. Wakati wa kufaa kuvuna samaki bwawani hutegemea
ukuaji na aina ya samaki. Ukuaji wa samaki pia hutegemea ubora wa
chakula. Samaki wanaofugwa katika bwawa lenye hali nzuri watakuwa tayari
kuvunwa baada ya miezi 6 hadi 8. Kuna watakao sema huu ni muda mrefu,
ukiona ufugaji wa samaki wanatumia muda jaribu kingine. Ama endelea
kukaa nyumbani kwako, ukiisubiri serikali na mashirika ya kijamii
yakusaidie.
Nielezee
kwa kifupi jinsi ufugaji wa samaki unavyochangia ajira binafsi kwa
watanzania na faida yake kwa ujumla. Changamoto mbalimbali za kiuchumi,
na ukosefu wa ajira kwa wasomi wanaotoka vyuo vikuu kwa sasa,
imesababisha watanzania wengi kuanza kuwa wabunifu na kuanza
kujishughulisha na ujasiriamali hasa kilimo na ufugaji. Kwa sasa mabwawa
mengi yanapatikana katika mikoa sita yenye rasilimali nyingi kama
Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Iringa, Mbeya na Ruvuma. Ufugaji wa
samaki umeenea kote nchini.
Kwa
sasa kilo moja ya samaki huuzwa shilingi 7,000/ kwa huku Iringa na
ukiuuzia bwawani kwa jumla ni shilingi 4000/ kwa kilo. Hii ina maana
kwamba ukiwa na kilo mia 7 za samaki una uhakika wa kuwa na milioni
mbili na laki nane kila baada ya miezi sita, kama utauzia bwawani kwa
bei ya shilingi elfu 4 kwa kilo ambapo hii ni samaki watatu tu aina ya
sato, je ukiwa na samaki ama kilo elfu tano? Utagundua kwamba adui wa
mafanikio yako ni sentensi za kizamani ulizo weka kichwani kwako.
Niseme
wazi tu kwamba, ufugaji wa samaki, ni fursa nyingine ambayo ipo wazi
kwa kila Mtanzania kuifanya, kuna watakao singizia mitaji, hali ya hewa
nk,lakini ukweli ni kwamba bwawalangu dogo nilitumia pesa ndogo sana
kulichimba ikiwa ni pamoja kununua vifaranga vya samaki.
Tumekuwa
watu wa kujiwekea mipaka ya mafanikio vichwani mwetu. Kumbuka kwamba
ukishajiwekea mipaka ya mafaniko. Maisha yetu yataweza kubadilika iwapo
tutabadilisha namna tunavyoyatazama mambo. Kwa mfano unaweza kuwa
umejiwekea mipaka ya kimapato kwamba wewe mwisho wako ni kupata laki
moja, mtazamo huo ukikaa kichwani basi ukiambiwa bwawa moja linaweza
kukutolea shilingi milioni 25 kwa miezi sita, utakataa na hivyo fursa
hiyo itakupita.
Nilipokuwa
nikisoma kitabu cha ‘THE TRUTH SHALL MAKE YOU RICH’ cha reallionaire
mdogo kuliko wote Farrah Gray kwa sasa, nimejifunza kwamba, maisha yetu
yanaweza kubadilika muda wowote na dakika yoyote iwapo tutajijengea
Imani kwamba, maisha yanawezekana popote. Na kwa Tanzania hii ambapo
kila mwananchi anaruhusiwa kulimiliki ardhi kwenye mkoa wowote umasikini
litakuwa ni swala la kujitakia.
Ninamalizia
makala hii kwa kusema kwamba, kila saa katika maisha yetu ni fursa,
makala hii pia ni fursa kwako na kwangu, kuna baadhi ya nchi duniani
ambapo wananchi wake hawana bahati ya kukaa kwenye meza zao na kujifunza
mambo haya. Kwawatakao penda kuja Iringa, kujifunza ufugaji wa samaki,
tunawakaribisha sana. Nicolaus na mimi na wafugaji wengine watakusaidia
kuapata elimu Zaidi yahii niliyoandika hapa.
No comments:
Post a Comment