Kamati ya Taifa ya Mbegu (National Seed Committee) imeidhinisha matumizi ya aina 29 za mbegu mpya za mazao mbali mbali ya kilimo. Mazao hayo ni mahindi, mpunga, alizeti, karanga na chai. Hatua hiyo ya Kamati inalenga kuongeza tija na kipato kwa mkulima.
Kuidhinishwa kwa aina hizo za mbegu kunafuatia mapendekezo yaliyofanywa na Kamati ya Taifa ya Kupitisha Aina Mpya za Mbegu za Mazao (The National Variety Release Committee) katika kikao chake kilichofanyika makao makuu ya Wizara ya Kilimo Mifugo na Uvuvi Dar-es-saalam tarehe 16 na 17 Machi 2016.
Aina hizo mpya za mbegu zimepitishwa baada ya kufanyiwa utafiti na kugundulika kuwa zina sifa mbalimbali kama vile kutoa mavuno mengi, kustahimili ukame, ukinzani dhidi ya magonjwa na wadudu, kukomaa mapema na kupendwa na wakulima.
Kati ya aina hizo mpya za mbegu, kuna aina 16 za mahindi, 2 za mpunga, 4 za alizeti, karanga 3 na 4 za chai. Mbegu hizo zimefanyiwa utafiti wa kina na vituo vya utafiti vya Umma na sekta binafsi hapa nchini kama ifuatavyo:-
TAASISI/KAMPUNI
|
ZAO
|
AINA YA MBEGU
|
Kituo cha Utafiti Seliani
|
Mahindi
|
· SELIAN H215
|
Kituo cha Utafiti Naliendele
|
Karanga
|
· NARINUT 2013
· NACHI 2013
· KUCHELE 2013
|
Kituo cha Utafiti Ilonga
|
Mahindi
|
· WE4102
· WE4106
· WE4110
· WE4114
· WE4115
|
Kituo cha Utafiti Tumbi
|
Mahindi
|
· T104
· T105
|
Kituo cha Utafiti Chollima Dakawa
|
Mpunga
|
· CH-SAT01
· CH-SAT09
|
Taasisi ya Utafiti wa Chai Tanzania
|
Chai
|
· TRIT201/16
· TRIT201/43
· TRIT201/44
· TRIT201/55
|
Sunflower Development
Company (SDC)
|
Alizeti
|
· NSFH36
· NSFH145
|
Advanta Seed Company Ltd
|
Alizeti
|
· AGUARA 4
· HYSUN 33
|
Meru Agro-Tours & Consultancy Co. Ltd
|
Mahindi
|
· MERU LISHE 503
· MERU LISHE 511
|
IFFA Seed Co Ltd
|
Mahindi
|
· KASPIDI HYBRID
· KISONGO HYBRID
|
Krishna Seed Co Ltd
|
Mahindi
|
· KRISHNA HYBRID-1
· KRISHNA HYBRID-2
|
Aminata Quality Seeds &
Consultancy Ltd
|
Mahindi
|
· NATA H 401
· NATA K8
|
Sifa za aina hizo mpya za mbegu zilizoidhinishwa na Kamati ya Taifa ya Mbegu
zimeambatanishwa katika Kiambatisho Na.1.
Aina hizo za mbegu zitaanza kuzalishwa na makampuni mbalimbali ya uzalishaji mbegu pamoja na Wakala wa Taifa wa Mbegu za Kilimo (Agricultural Seed Agency - ASA). Lengo ni kuzifikisha aina hizo mpya za mbegu bora kwa wakulima kuanzia msimu wa 2017/2018.
No comments:
Post a Comment