Saturday, June 3, 2017

KILIMO BORA CHA DENGU

UTANGULIZI
Dengu ni zao la chakula na biashara lenye kiasi kikubwa cha protini, vitamini A na B, Madini ya Potassium na chuma. Zao hili likilimwa vizuri linaweza kutoa mavuno ya kilogram 200 hadi 500 kwa ekari. Zao hili huchukua wastani wa siku 135 kupandwa hadi kuvunwa.
HALI YA HEWA NA UDONGO
Ni zao linalohitaji hali ya hewa ya kibaridi kiasi kwani joto kali na ukame sana huathiri mavuno yake, hupunguza wingi wa mavuno. Ni zao linalostahimili ukame, linaweza kukua katika hali ya hewa ya unyevunyevu tu. Kama utakuwa unamwagilia basi epusha unyevu mwingi ikifikia kipindi cha maua hadi kuvuna. Zao hili linaweza kulimwa katika udongo wa aina tofauti tofauti wenye Ph 6-8. Udongo wenye asidi na base kidogo. Kwa Tanzania zao hili linaweza kulimwa katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Mwanza, Singida, Morogoro, Shinyanga N.K. Lakini kwa sasa mikoa ya Shinyanga na Mwanza ndio wazalishaji wakubwa wa dengu.
UPANDAJI NA NAFASI
Zao hili huitaji mbegu kiasi cha kilogram 15 hadi 40 kutegemea ukubwa wa mbegu husika. Zao hili hupandwa mwishoni mwa msimu wa mvua,unaweza kupanda baada ya kuvuna mazao mengine uliyopanda mapema, Mbegu za dengu hufukiwa katika kina cha sentimeta 5 hadi 6 ili kufanya mazingira rafiki kwa bacteria wa rhizobia kufanya kazi. Zao hili usipande pamoja na vitunguu na tangawizi. Panda kwa kutumia drilling method-njia ya vifereji kwa nafasi ya mistari miwili ya sentimeta 15 na sentimeta 30 hadi 50 kwa mstari hadi mstari.
MBOLEA ZA VIWANDANI NA SAMADI. 
Mbegu unaweza kuzipanda baada ya kuziongeza inoculam kundi F na Pia Mbolea ya DAP kilogram 25 hadi 50 kwa ekari katika shamba lisilo na rutuba ya kutosha.
PALIZI-Palilia mapema shamba lako.
WADUDU WAHARIBIFU KWA DENGU 
Dengu hushambuliwa na Mchwa wakubwa weusi, aphid wa njegere, funza wa vitumba, Inzi wa lucina n.k wazuie wadudu hawa kwa kupuliza dawa za wadudu mara tu uonapo dalili za mashambulizi ya wadudu.
MAGONJWA YA DENGU 
Dengu hushambuliwa sana na magonjwa ya ukungu ambayo. Hivyo kama eneo lako hushambuliwa na ukungu mara kwa mara basi puliza dawa za ukungu (FUNGICIDES)
UVUNAJI WA DENGU Zinavunwa mara tuu pindi vitumba vya chini vibadilikapo rangi kuwa kahawia angavu na vitumba vikiguswa hutoa sauti.
Ahsanteni sana! Endelea kujifunza.

1 comment:

  1. Enter your comment...nivizur kutupa maujuz yakujikwamua na umasikin

    ReplyDelete