Monday, June 5, 2017

kumfunga mbuzi kamba shingoni Ni hatari




Kufunga kamba mbuzi humsababishia kudhoofika na kupunguza uzalishaji. Pia, ni rahisi kwa mbuzi aliyefungwa kamba kushambuliwa na wadudu ambao matokeo yake ni magonjwa ya mara kwa mara, jambo ambalo litaathiri kipato cha mfugaji.

Mbali na magonjwa, mbuzi anapofungwa kamba anaweza kuvunjika shingo na kufa, au kuumia vibaya.
Inapotokea akashtuka au kutaka kukimbia anapotokea mnyama kama vile mbwa, mbuzi atajaribu kukimbia.
Hivyo, kamba aliyofungwa shingoni kumuumiza. Pia ni rahisi mbuzi aliyefungwa kuathiriwa na hali ya hewa kama vile jua kali au mvua inaponyesha, mbuzi hawezi kukimbia kujikinga dhidi ya mvua au jua.

Ni dhahiri kuwa wafugaji wengi wana bidii sana na kuwa na matumaini makubwa kutokana na kazi zao. Hari ya kuwa na uzalishaji mzuri kutokana na mifugo yao pia ni dhahiri.

Pamoja na hari hiyo, wafugaji wengi wamekuwa hawazingatii kanuni bora za ufugaji na utunzaji wa mifugo yao. Mbuzi wa aina zote wawe wa kisasa au kienyeji wana tabia ya kupenda uhuru na wanahitaji matunzo mazuri ili kuwa na ufanisi mzuri.

Endapo ni lazima kuwafuga mbuzi nje ya banda, ni vyema wakatengewa eneo la wazi ambalo litawapa uhuru wa kutembea huku wakila majani. Ni vizuri mfugaji akajifunza na kuzingatia njia bora za ufugaji wa mbuzi wa maziwa ili kuepuka kufuga kwa mazoea na kutopata faida halisi.

No comments:

Post a Comment