Saturday, June 10, 2017

NJIA BORA ZA KUKINGA MIMEA YAKO DHIDI YA JUA KALI NA MVUA KUBWA


Mara baada ya kujua kuhusiana na mbolea ya maji na mbolea nyinginezo pamoja  na aina za umwagiliaji na kilimo hiki cha kisasa kwa ujumla tunafaidika sana na nakala zako za kilimo sana. Kwa ujumla naitwa Saida Salumu kutoka Tanga Tanzania nahitaji kujua ni jinsi gani naweza kuepuka hasara inayosababishwa na jua kali au mvua kali katika kilimo changu.

MAJIBU;
KUKABILIANA NA JUA
Jua kali utakabiliana nalo kwa kujua aina ya udongo ulionao mfano kama udongo wako unahifadhi sana maji na jua kali lipo ila bado uhifadhi wa maji ni mkubwa hapa utapaswa kukabiliana na hali hii kwa kumwagilia mara moja kwa siku moja ili kuepukana na ugonjwa wa kata kiuno. Ila kama udongo unahifadhi maji na jua likawa kali kiasi ambacho saa sita mchana maji yashakauka na mmea unaanza kusinyaa au kuweka rangi ya njano kutokana na jua kali hapo inabidi ukabiliane na changamoto hii kwa kufanya yafuatayo:-
a.      Kuweka matandazo ya majani (Organic mulch)


b.      Kuweka matandazo ya plastiki (Plastic mulch) wasiliana na sisi tukupatie
c.       Au kuweka kichanja kama ni bustani ndogo ya mboga mboga
d.      Kufunga mfumo wa umwagiliaji kwa njia ya matone pamoja na njia ya matandazo pia. Hapa kama mkulima waweza kabiliana na jua na ukafanya kilimo chenye tija. Bila kufanya haya mmea wako utatoa mazao madogo, au kusinyaa au kubadilika rangi na kuwa wa njano na kudumaa pia. Kumbuka mmea kabla ya kubakia na maji yatayotumika na mmea kuna kiwango maalumu cha maji yanayopotea hewani kwa njia ya stomata. Na hapa mmea unapaswa kubaki na kiwango cha maji ambayo yatatumika na kazi muhimu mbali mbali kwa mmea wako. Njia nlizoeleza pale juu zitausaidia mmea wako kuhifadhi unyevu kwa matumizi ya mmea.
KUMBUKA: Kila mmea una mahitaji maalumu ya mwanga na maji.
NET MAALUMU KWA AJILI YA MABANDA KITALU

Lakini pia upande wa pili kujikinga na jua kali japo njia hii itakusaidia kujikinga na mvua yenye madhara  hapa unaweza kujenga Banda kitalu (Green House), au Net house jengo ambalo tumelieleza vyema sana katika nakala zilizopita faida na hasara zake. Hili jengo husaidia kwa kiasi kikubwa katika kupunguza mionzi ya jua na mtone ya mvua. Lakini pia kuna majengo mengine ambayo yataweza kutumika kupunguza miale mikali ya jua kama kichanja house, net house faida ya majengo haya hupunguza miale ya jua na mvua japo net house huingiza maji. Kwa ujumla maeneo ya pwani jua huwa kali sana hivyo basi mkulima napaswa kuzingatia haya ili aweze kufanya kilimo chenye tija.
KUHUSIANA NA MVUA
Kama mkulima mvua ina faida kubwa sana hasa ikanyesha kipindi ambacho ndo unaotesha au kipindi amacho ndo unahamisha mazao yako shambani kutoka kitaluni. Kikubwa jitahidi kujua aina ya zao lako na uhitaji wake wa maji. Kumbuka uhitaji wa maji kwa kila mmea hutofautiana. Ukiachilia mbali kuwa uhitaji tofauti tofauti wa maji kwa kila mmea. Maji yakiwa mengi huleta madhara yafuatayo:-
Magonjwa ya fangasi, mfano mmea kukata kiuno (Damping Off), ugonjwa wa ukungu ambao ni hatari sana, na magonjwa mengine ya kuozesha tunda (Fruit end root) japo ugonjwa huu wa kuoza tunda wakulima wengi hujua sababu moja tu ya kukosekana madini ya kalshamu lakini pia ikitokea huna ratiba maalumu ya umwagiliaji pia ugonjwa huu utakupata haswa mvua ikianza kunyesha huwa inanyesha kipindi tofauti tofauti sana na hivyo huleta madhara moja kwa moja.
SWALA LA KUFANYA

Ni muhimu sana unapoona muda mwingi kuna mawingu na mionzi ya jua ni hafifu, basi ni muhimu sana kutafuta dawa zenye kiambata cha KOPA (Copper) mfano Blue Copper, au Red Copper, au dawa kama Ivory, Ebony 72 WP, hizi dawa zoote zenye copper husaidia mmea kuwa wa moto, hivyo kupunguza fungus kujijenga.Fungus hupenda hali ya unyevu unyevu.. kwa mfano katika zao la kahawa inashauriwa sana katika kuzuia ugonjwa unaoitwa Coffee Berry Diseases-CDB, ugonjwa wa kunyauka matunda, ni vizuri mkulima akapiga dawa za kuzuia ukungu mwezi mmoja kabla ya mvua kuanza, ili kuupa mmea moto, lakini wakulima wengi hawafanyi hivyo. Huwa wanasubiri hadi wavamiwe ndio wapige, lakini ugonjwa kama huo CBD ukivamia mkahawa hakuna jinsi utafanikiwa kuupunguza ndo hapo ambapo unakuta sasa mkulima anapata hasara kubwa kwa kuwa mashambulizi yanakuwa ni makubwa sana ya mdudu huyo. Hii pia ipo kwa mazao mengine kwa hivyo mkulima ajue jinsi ya kuukinga mmea wake na ukungu. 

No comments:

Post a Comment