Wednesday, June 14, 2017

Tuanze kufuga bata

Bata ni aina ya ndege wafugwao wanafanana sana na kuku lakini watu wengi hasa Watanzania wanaamini kuwa nyama ya bata imepooza lakini ukijaliwa kutembelea nchi ya Uholanzi mgeni aliyeheshimiwa hukaribishwa nyama ya bata na bei yake ni aghali ukilinganisha na kuku. Ufugaji wa bata ni rahisi ukilinganisha na wa kuku kwani hawashanbuliwi sana na magonjwa na chakula chake hupatikana kirahisi pia wanawezwa kufugwa ndani ya ua au banda.

Ni vizuri sasa watanzania wakahamasika kufuga bata kwani kilishe hana tofauti na kuku. Bei ya bata hapa Dar es Salaam ni kati ya Tshs 20,000-30,000/=

1 comment:

  1. Nimeanza ufugaji wa bata huu ni mwaka unamalizika. Nilinunua bata 25 lakini kwa bahati mbaya sina elimu ya kutosha juu ya ufugaji wa bata. Kuna bata 2 ambao wameangua @ vifaranga5 wanekufa wamebaki 4.
    Kuna ambaye ana vifaranga 12 naona anaendelea vizuri. Kuna ambaye ameacha kuatamia sikujua sababu naona kama mayai yameshaharibika. Huyu aliyeharibu mayai sikugusa wala kusogeza mazingira ambayo alitagia mayai. Naomba ushauri kwa anbaye ana uzoefu.

    ReplyDelete