Saturday, July 1, 2017

Ufugaji wa kisasa wa samaki: Utaalamu na Masoko

Tujifunze kuhusu ufugaji wa samaki wa kisasa ambao hufanyika kwenye mabwawa ya kuchimbwa au visima na vitu vingine vinavofanana na hivyo.

Kuna aina nyingi za samaki wa maji baridi ambao wanaweza kufugika kwa urahisi au ugumu kidogo tu na aina hizo wapo wale ambao sio wa kuzaliana(monosexual) na wale wa kuzaliana(heterosexual)

Urahisi hapa uko zaidi kwenye kuwafuga wasiozaliana sababu hawaongezeki wakati wale wanaozaliana utakuwa na utaratibu wa kuhamisha fishling(vifaranga) sehemu nyingine.

Rasilimali muhimu za kuwa nazo ili kufanikisha shughuli hii ni eneo la ardhi,maji, rasilimali watu na rasilimali fedha.Eneo la ardhi ndio litakaloonyesha ni kwa namna gani bwawa lako liwe,aidha la kujengea na cement,kutandika plastic au kuchimba na kulitumia hivyohivyo.Bwawa huchimbwa/kujengwa kwa kuwa na sakafu yenye ulalo kiasi(gentle slope/gradient)

Wapo samaki aina ya Sato(Tilapia),Kambale(African catfish) na wengine aina ya pangasius ambao hufugwa kwa wingi sana.
Unahitaji samaki 7-8 katika meter moja ya mraba(1m^2) ,kwa maana hiyo kama una meter za mraba 600 nasi unaweza kufuga samaki 4500.Haishauriwi kulundika samaki kwenye eneo dogo kwani itawasababishia ukosefu wa hewa(oxygen).Ingawa zipo njia za kuweza kuongeza upatikanaji wa hewa kwenye mabwawa.

Ukishachimba bwawa lako(aidha na kulijengea) unaingiza maji kwenye bwawa hakikisha yamekaribia futi 2.5 mpaka kujaa full.Itakubidi kufanya liming(kumwagia chokaa bwawa kabla ya kuweka maji ili kuua bacteria hatarishi kwa maisha na afya ya samaki wako) pia unahitajika kuyarutubisha hayo maji kwa kuchanganya na mbolea(kama ya ng'ombe na za viwandani pia ingawa haishauriwi sana) na kusubiria kwa muda usiopungua siku 21 au zaidi.Unafanya hivi ili kuweka mazingira ya chakula asili(natural foood) kwa ajili ya samaki kujitengeneza,vyakula hivo hua katika hali ya mimea na viumbe wadogo(microorganisms)

Upatikanaji wa vifaranga vya samaki,hapa inakubidi uwe makini sana kama umeamua kuzalisha sato,changamoto kubwa ya sato ni kupata mbegu ambayo under right conditions vifaranga vitaweza kua samaki wenye uzito wa kutosha(miezi 6 awe at least 500grams au zaidi).Mbegu ya sato hupatikana kwa bei rejareja ya sh 300 na kambale sh 500 kwa kifaranga kimoja.Wapo wazalishaji wengi wa mbegu za vifaranga wa ndani na nje ya nchi ila kwa Tanzania nimewakubali Tanzania Fisheries Research Institute(TAFIRI) Nyegezi,Mwanza(Nimefwatilia performance yao shambani).

Ulishaji wa vifaranga vyako ,chakula chao kinategemea na uzito wao mfano samaki hula 5% ya uzito wake wa mwili akiwa mdogo na 3% akiwa mkubwa.Hapa tunaongelea ulishaji wa chakula cha ziada(supplement food),sababu cha asili amekipata kwenye ile mbolea ulioweka.Kama una vifaranga 100 vyenye gram 10 kila kimoja basi utahitaji gram 50 kuwalisha.

Itakuchukua Miezi 6-9 kuanza kuvuna samaki wako ambao unaweza kuwauza kulingana na uzito au au njia utayoona inakufaa.Samaki wengi wa kwenye mabwawa wanavunwa kwa kutumia nyavu au kumwaga maji yote nje ya bwawa.Masoko yake haya samaki ni pamoja na supermarkets, wafanyabiashara sokoni na mitaani pamoja na watu binafsi.

No comments:

Post a Comment