UTANGULIZI
Mchicha ni mojawapo ya mboga za asili ambayo hulimwa katika mikoa yote hapa nchini. Mboga hii ina vitamin A, C, na madini aina ya chokaa na chuma kwa wingi Majani ya mchicha huliwa baada ya kupikwa au kutengenezwa supu. Mbegu zake zinaweza kusagwa na kupata unga unaoweza kutumika katika mapishi mbalimbali kama vile kutengeneza ugali, uji, chapati na maandazi.
MAZINGIRA
Mchicha unaweza kulimwa karibu katika aina yeyote ya hali ya hewa na kwenye udongo wa aina yeyote ili mradi usituamishe maji. Udongo wenye rutuba nyingi unafaa zaidi kwa ustawishaji wa zao hili.
AINA
Kuna aina nyingi za mchicha; zifuatazo ni aina zinazostawi hapa nchini:-
- Mchicha Mweupe
Aina hii ina majani marefu yenye rangi ya kijani ya kupauka. Huvunwa kwa kung'oa na huuzwa sana sokoni. - Mchicha Mpana
Ni ule ambao ni mnene na una majani mapana na yenye rangi ya kijani kibichi. Huweza kuvunwa kwa kurudiwarudiwa - Mchicha Mwembamba
Huu ni mdogomdogo na unaota shambani kama gugu. Majani yake ni madogo na huchanua mapema. - Mchicha wa Unga
Mchicha huu huwa mwekundu unapokuwa mdogo na hukua haraka. Hutoa mbegu nyingi ambazo zinaweza kusagwa unga, ambao unaweza kutumika kutengeneza vyakula mbalimbali kama vile, uji na maandazi. Majani yake hupikwa kama mboga au hutengenezwa supu.
Tayarisha shamba mwezi mmoja kabla ya kupanda. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri ili kuongeza rutuba ya udongo. Mbolea hizi pia hufanya udongo ushikamane vizuri na kuhifadhi unyevu kwa muda mrefu. Weka kiasi cha ndoo moja yenye ujazo wa lita ishirini katika eneo la mita mraba mmoja. Changanya vizuri mbolea hii na udongo. Wiki mbili kabla ya kupanda laininsha udongo na sawazisha udongo.
KUPANDA
Kuna niia kuu mbili za kuoanda mchicha, Kupanda mchicha moja kwa moja shambani na kuotesha miche kwanza kwenye kitalu.
- Kupanda Moja kwa Moja Shambani
Mbegu hupandwa moja kwa moja kwenye shamba la kudumu na baadaye mimea hupunguzwa na inayobaki huachwa katika nafasi ya sentimita 15 hadi 23. Mbegu huweza kupandwa katika sesa au matuta. Kiasi cha kilo moja hadi mbili za mbegu kinatosha kuotesha katika eneo la hekta moja. Ili kuepuka mlundikano wa mbegu sehemu mmoja, changanya mbegu na mchanga kwa kiasi kinacholingana kabla ya kumwaga shambani. Kisha mwaga na funika kwa kiasi kidogo cha udongo au mbolea laini za asili. Tandaza nyasi kavu na mwagilia maji. Endelea kumwagilia kila siku asubuhi na jioni hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku tatu mpaka tano na baada ya kuota ondoanyasi. - Kuotesha Miche Kwenye Kitalu
Kutayarisha Kitalu:
Sehemu itakayooteshwa mbegu inatakiwa iwe laini na yenye rutuba ya kutosha. Hivyo baada ya kulima lainisha udongo kwa kupigapiga mabonge makubwa. Kisha tengeneza tuta lenye upana wa mita moja na urefu wowote. Weka mbolea za asili zilizooza vizuri kiasi cha debe moja au mbili katika kila eneo la mita mraba moja. Changanya mbolea hii na udongo vizuri, kisha sia mbegu zilizochanganywa na mchanga kwenye mistari yenye nafasi ya sentimita 10 hadi 15. Baada ya kusia, funika mbegu kwa kiasi kidogo cha udongo au mbolea laini za asili. Weka matandazo na mwagilia maji. Endelea kumwagilia kila siku asubuhi na jioni mpaka mbegu zitakapoota. Baada ya siku 4 mpaka 6 ondoa matandazo na endelea kumwagilia maji.
KUHAMISHA MICHEBaada ya wiki mbili miche inakuwa tayari kwa kupandikizwa shambani. Wakati huu huwa na majani mawili mpaka manne. Mwagilia kitalu siku moja kabla ya kung'oa miche ili kueipusha mizizi isikatike. Ng'oa miche kwa uangalifu na pandikiza katika kina cha sentimita tetu na nafasi ya sentimita 30 hadi 38 kati ya mstari na mstari. Nafasi kati ya shimo na shimo iwe sentimita 15 hadi 22 Aina ya mchicha mayokua sana ipandikizwe sentimita 60 toka mche hadi mche na sentimita 60 mstari hadi mstari. Baada ya kupandikiza mwagilia shamba kama hali ya hewa ni yajua kali.
Palizi
Ni muhimu kupalilia shamba mara kwa mara ili kuondoa magugu.
Kumwagilia
Mwagilia kila siku asubuhi na jioni hasa wakati miche bado michanga.
Mbolea
Mbolea ya kukuzia (S/A) huwekwa kila baada ya siku 10 hadi 14. Kiasi kinachohitajika ni gramu tano (kijiko kimoja cha chai) kwa kila mche. Kama mbolea aina ya Urea itatumika, weka nusu kijiko.
Wadudu Waharibifu na Magonjwa:
Wadudu
- Utiriri (Red Spidermites)
Ni wadudu wadogo sana ambao wana rangi ya machungwa yaliyoiva, nyekundu au kahawia. Huonekana upande wa chini wa majani na hushambulia kwa kufyonza utomvu wake. Majani yaliyoshambuliwa huwa njano, husmyaa, hujikunja na hatimaye hukauka. Wazuie wadudu hawa kwa kunyunyizia moja ya dawa zifuatazo: Dimethoate, Politrin, Selecron (Profenofos) na Ekalux. - Vidukari au Wadudu Mafuta (Aphids)
Hawa ni wadudu wadogo wenye rangi ya kijani, nyeusi au kahawia. Hushambulia mchicha kwa kufyonza utomvu wa majam machanga. Mmea ulioshambuliwa hudhoofu, hudumaa na hatimaye hufa. Di kuzuia vidukari, tumia dawa kama vile Dimecron, Dimethoate, Actellic 50% E.C, Diclorvos na Sumicidin. - Mbawakau (Leaf Eating Beetles)
Wadudu hawa wana mabawa magumu kama yaliyokauka Hushambulia majani na kuyasababisha yawe na matundu Waangamize wadudu hawa kwa kunyunyizia dawa kama vili Carbaryl (Sevin), Actellic 50% EC, Sumithion, na Dimethoate - Kijambisi/Kinyafungo (Green Stinkbug)
Mdudu huyu ana rangi ya kijani kibichi na hunuka vibaya Hufyonza utomvu wa mimea michanga na mbegu changa Mbegu zilizoharibiwa huwa mapepe. Tumia mojawapo ya dawa zifuatazo kumzuia mdudu huyu; Decis, Carbaryl Sumithion na Dimethoate. - Sota (Cutworm)
Hawa mfano funza wakubwa wenye rangi ya kijivu ambao hukata miche karibu na usawa wa ardhi. Hujificha ardhini mchana na kutoka usiku kukata miche iliyoko kitaluni au iliyopandws muda huo huo. Wazuie wadudu hao kwa kutumia dawa ya Sevin, au Sumithion. Weka dawa kwenye udongo au ndani ya shimo kabla ya kupandikiza miche.
- Kinyawhi (Damping off)
Ugonjwa huu husababishwa na ukungu na hushambulia miche michanga kwenye shina usawa wa ardhi. Shina lililoshambuliwa hukauka na hatimaye mmea wote hunyauka nakukauka.
Ugonjwa huu unaweza kuzuiwa kwa kuzingatia yafuatayo:-
- Punguza miche ili kuruhusu hewa ya kutosha
- Epuka kumwagilia juu ya mimea
- Tumia dawa za ukungu kama vile Dithane M 45, Ridomil, Topsin - M.
Hii hufanyika kwa mchicha ambao hauvunwi moja kwa moja. Ondoa vichwa vya maua ili mimea iweze kutoa machipukizi mengine pembeni ambayo yataongeza mavuno.
KUVUNA
Mchicha huwa tayari kwa kuvunwa katika wiki ya tatu hadi sita tangu kupanda. Uvunaji unaweza kufanywa kwa kung'oa au kwa kukata majani yajuu, na kuacha mashine yaendelee kuchipua tena. Kila unapokata weka mbolea za kukuzia (S/A au Urea) ili kuongeza ukuaji wa machipukizi. Pia endelea kumwagilia maji.
Mchicha uliotunzwa vizuri huendelea kuvunwa kwa muda wa miezi mitatu au zaidi. Wastani wa mavuno m tani 20 hadi 40 kwa hekta. Mchicha kwa ajili ya mbegu huvunwa baada ya mbegu kukomaa au miezi mitatu tangu kupandwa. Baada ya kuvunwa,, masuke hukaushwajuani na baadaye mbegu hutenganishwa.
HIFADHI
Mchicha kwa ajili ya matumizi ya baadaye huweza kuhifadhiwa kwa kufungwa kwenye kitambaa cheupe na kutumbukizwa kwenye maji ya moto yenye chumvi kwa muda wa dakika moja. Baada ya hapo huanikwa juani.
Hifadhi mboga iliyokaushwa kwenye vyombo safi kama vile vibuyu, debe, vikapu na mifuko ya plastiki.
No comments:
Post a Comment