Thursday, June 15, 2017

UMUHIMU WA KULIMA MAZAO YA CHAKULA

UMUHIMU WA KULIMA MAZAO YA CHAKULA


Mazao ya chakula ni mazao ya muhimu katika kuishi kwa kila siku kwa mwanadamu.Hivyo hayana budi kulimwa kwa wingi katika misimu ya kilimo ili kuepuka baa la njaa. Mazao haya ya chakula yamegawanyika katika makundi makuu mawili.

1.MAZAO YA CHAKULA YANAYOSTAHIMILI UKAME

Haya ni mazao ambayo yanaweza kulimwa katika maeneo yapatayo mvua chache au yenye mvua za msimu zinazonyesha kwa muda mfupi.Mazao haya ni muhimu sana katika kukabiliana na baa la njaa.Mazao haya ni kama vile MTAMA WA MUDA MFUPI,MUHOGO,UWELE,MAHINDI YA MUDA MFUPI (TMV's),MBAAZI,CHOROKO n.k.

2.MAZAO YA CHAKULA KWA UJUMLA


Mazao haya yanaweza kulimwa katika maeneo mchanganyiko yapatayo mvua nyingi na  wastani Mazao haya ni Kama vile MPUNGA,MAHINDI,MTAMA,NDIZI,MAHARAGE,VIAZI MVIRINGO NA VITAMU n.k.

UMUHIMU WA MZAO HAYA KATIKA JAMII

Jamii kubwa kwa sasa imepunguza ulimaji wa mazao haya  na kusababisha upungufu wa mazao haya na vile vile ongezeko la bei katika mazao haya.Siku hizi haishangazi kukuta wakulima wenye ardhi nzuri na inapata mvua ya kutosha kulima mazao haya lakini wanajikita zaidi katika ulimaji wa mazao ya biashara na wakijikuta baada ya muda mfupi wakiwa watumwa wa wafanyabishara wa mazao ya chakula kununua na kwa bei isiyo rafiki kwao bidhaa kama vile MCHELE na UNGA ambapo wangeweza kuzalisha wenyewe na kuokoa kiasi kikubwa cha matumizi ya Pesa.
Mazao ya chakula yakilimwa na wakulima wenyewe yanaweza kuondoa au kupunguza  yafuatayo katika jamii (kaya zao)
       1..kuwa na uhakika wa chakula majumbani hivyo Kuuondoa au Kupunguza baa la njaa
        2...Kupunguza Matumizi makubwa ya Pesa kununulia chakula.
         3....Kuzuia mfumuko wa bei wa mazao ya chakula katika jamii hiyo
         4....Kuwezesha serikali kupeleka matumizi ya pesa katika huduma nyingine muhimu                                                                                                                                            
                  badala ya kupeleka katika kuokoa njaa 
       5....Kuwa na jamii yenye afya bora 
         6......Kupunguza wizi mdogomdogo wa mashambani  n.k 

NINI CHA KUFANYA TUKIWA KAMA WANAJAMII NA WAKULIMA

Ili tuondokane na baa la njaa ambalo linaweza likaepukika basi inabidi kwa pamoja tuwashauri wezetu hasa vijijini wakubali kubadilika kutokana na mabadiliko ya tabia nchi (mabadiliko ya hali ya hewa) na walime mazao ya chakula ambayo yanaweza kupambana kwa kiasi kikubwa na mabadiliko hayo. Mfano kuna maeneo hawali mtama au muhogo lakini mazao haya yanaweza kulimwa na yakaokoa njaa lakini wakazi hawayataki kutokana na utamaduni wao wa asili au uliliobadilika na kuwafanya kutokula mazao hayo kama chakula hivyo kuyagomea kulima na kukubali Kupanda mazao ambayo Baadaye yanaweza yasifike mwisho na kuwasababishia njaa au Wengine wanakula lakini Hawalimi mazao haya Na Kuamua kulima mazao ya Biashara tuu wakishayauza wanabaki hawana chakula bali pesa ambayo haitabiriki mfukoni Mwishowe hujikuta kushindwa kuhimili ununuzi wa mazao  chakula sokoni na madukani. HIVYO kwa pamoja inabidi tushauriane na tuwashauri wakulima wenzetu hasa vijijini walime mazao ya chakula kwa wingi na hasa yanayostahimili ukame na wayahifadhi vizuri kwa ajili ya chakula.Pia walimapo mazao ya biashara wasisahau kulima mazao ya chakula pia.

'''HESHIMA NA TABIA NA AFYA NA MWALIMU WA HESHIMA NA TABIA NA AFYA KATIKA NYUMBA wa KWANZA NI CHAKULA-PANAPOKOSEKANA CHAKULA MENGI HUZALIWA"""


      HAPA KILIMO TUU-NDO AJIRA NA KAZI NA BIASHARA

No comments:

Post a Comment