Wednesday, September 27, 2017

Matunzo Ya Kuku Kuanzia Siku Ya Kwanza Unapowachukua Mpaka Siku Ya 90 Au Miezi 3

1. Utayarishaji wa banda.
i. Banda liwe safi, lisafishwe lisiwe na vumbi.
ii. Pulizia dawa ya kuondoa viroboto, utitiri na chawa kwa kutumia dawa kama Ectomin Dip.
ii. Pulizia dawa ya kudhibiti wadudu wasababishao magonjwa, tumia disinfectant mfano Vivid/TH4.

Tayarisha taa na moto (charcoal) kwa ajili ya kuweka chumba kiwe na joto la kutosha.

SIKU YA 1.
                 i.  Vifaranga wanapofika tu wapewe Glucose kwenye maji kwa masaa 8 mfululizo.

                ii. Baada ya hapo wapewe Vitalyte kwa siku 2 mfululizo.

SIKU YA 3.
                 Wapewe chanjo ya Newcastle Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie Vitalyte au Antistress kwa siku 3 mfululizo.

SIKU YA 7.
                Wapewe chanjo ya Gumboro Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie maji ya Antistress kwa siku 2 mfululizo.

SIKU YA 10.
                   Wapatie OTC Plus kwa siku kwa saa 24 kwa siku 3 mfululizo.

SIKU YA 14/18/19.
                  Wapatie Esb3 na Vitalyte kwa masaa 24 kwa siku 3 mfululizo.

SIKU YA 21.
                  Wanyweshe Newcastle Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie Antistress kwa siku 4 mfululizo.

SIKU YA 28.
                 Wapewe Gumboro Vaccines kwa saa 2 mfululizo. Baada ya hapo wapatie Antistress kwa siku 2 mfululizo.

SIKU YA 31.
                  Wapatie  OTC Plus kwa siku 7 mfululizo.

SIKU YA 43/44/45.
                  Wapatie Esb3  na Vitalyte kwa masaa 24 mfululizo kwa siku 3.

SIKU YA 50.
                 Wapewe chanjo ya Fowl Pox. Baada ya hapo endelea kuwapa Chickmycin au Chick Plus kwa wiki 2 mfululizo.

SIKU YA 65.
                  Chanjo ya Gumboro na baada ya hapo endelea na Antistress.

SIKU YA 69.
                  Wapatie dawa ya Minyoo mfano Levalap kwa siku 2 mfululizo.

SIKU YA 72.
                 Wapewe Fluquin kwa siku 5 mfululizo.

SIKU YA 79.
                 Wapewe Anticox na Vitalyte kwa siku 5 mfululizo.

SIKU YA 90.
                  Wapewe tena chanjo ya Newcastle Vaccines kwa saa 2 mfululizo.
Baada ya hapo endelea kuwapa Antistress kwa siku 3 mfululizo.


Hapo sasa endelea na Utaratibu wa kawaida wa chanjo na tiba.

No comments:

Post a Comment