Sunday, November 19, 2017

Faidika Kwa Kulima Kilimo Cha Figiri

Ulimaji wa mbogamboga hususani figiri  ni shughuli nzuri  hufanywa na baadhi ya watu wanao jikita katika kujipatia kipato. sasa leo nami nimependa kukupa somo mpendwa wangu kuhusu hiki kilimo.

Naam kilimo cha mboga mboga kinawatoa watu katika hali ya ukata na kuwapa maisha ya kati na hata wakati mwingine kuwapeleka katika ukwasi. Namaanisha shughuli hii itakupatia kipato cha kukidhi haja za kimaisha yako endapo utaamua kulima.

Tuangalie mambo muhimu katika kilimo hiki.

KUANDA SHAMBA / BUSTANI

  • Huwezi kulima pasipo kuanda shamba au bustani yako.
  • Namna ya kuanda shamba.
  • Lima shamba lako vizuri na kuondoa nyasi/ magugu yote yaliyoootea katika shamba. Kisha katua vizuri shamba lako kwa lengo la kuulainisha udongo wa shamba lako.


Baada ya hapo mwagia mbolea ya kutosha katika shamba lako kisha mwagilia maji ya kutosha kutengeneza unyevunyevu wa kutosha.

KUMWAGA MBEGU
Mbegu humwagwa katika bustani kwa kurusha. Lakini mbegu hizi kabla hazija mwagwa kwenye bustani lazima uchanganye na mchanga kwa lengo la kupatia nafasi pindi utakapo mwaga mbegu na kupelekea figiri kuota kwa mpangilio. Lakini pia ikumbukwe mbegu huota ndani ya siku 3. Tangu kumwagwa.

Utaendelea kumwagilia bustani yako kila baada ya siku 2. Kwa udongo wa tifutifu. Na kila siku kwa udongo wenye aina ya kichanga kwani aina hii ya udongo hu pitisha maji kwa urahisi na kukauka haraka.

Mboga hii huchukua siku 30. Kuwa tayari kwa kuuzwa na wateja kwenda kula.

Mpaka kufikia hapo hatuna la ziada, endelea kutembelea blog ya kilimo bora.

No comments:

Post a Comment