Saturday, October 13, 2018

KILIMO BORA CHA MACHUGWA






   UTANGULIZI.

    Mchungwa ni jamii ya mlimao, lakin hustawi zaidi ukandawa pwani wenye joto kiasi, mvua zaidi na udongo wenye rutuba. Hapa Tanzania mikoa kama Pwani, Dar es salaam, Tanga, Mtwara, Lindi, na Morogoro ni maarufu kwa kilimo hiki. Pia tunda la mchungwa huliwa na binadamu ili kuongeza vitamini mwilini.

Hali ya hewa.
Michungwa huweza kukuzwamaeneo yenye joto na hata yale yenye baridi. Kama ilivyo kwa matunda mengineya citrus, ili kupata mazao mazuri haina budi kukuza michungwa katika joto la nyuz ijoto 15.5c – 29c.

Kuandaa mbegu.
Mchungwa kwa kuanzia unakusanya mbegu za mlimao kutoka katika malimao yaliyokomaa na ikiwezekana yawe yameiva yakiwa mtini, kausha mbegu zake na kasha unaweza kutolea ganda la nje ili ziweze kuota vizuri.



Kuandaa kitalu.
Tengeneza kitalu chako vizuri kwa kutumia jembe, kisha changanya na mbolea za mboji au samadi baada ya kukauka vema mwaga mbegu zako na uzifukie kwa udongo kiasi cha nusu sentimita, kasha mwagia maji kila siku na baada ya wiki 3 - 6 mbegu zitaanza kichipua, baada ya miche kufikia kiasi cha sentimita 3 – 5, miche ihamishwe kwenye pakiti zenye udongo (viriba) wenye mbolea ya kutosha na viwekwe kwenye kivuli kiasi.

Kuunga miche.
Miche ikifikia urefu wastani wa sentimita 30 – 45 huungwa ili kupata michungwa. Kwa michungwa kuna aina mbili kuu hapa Tanzania ambazo ni Jaffer na Valencia. Jaffer ni rahisi kuunga sababu vikonyo vyake ni vikubwa na viko wazi kwenye miti, miti yake ni mikubwa na inazaa sanalakini huathirika sana jua likiwa kali na matunda yake huanguka, pia machungwa yake hukua kwa haraka sana ilasoko likiwa  baya huishia shambani kwa kuanguka. Vlencia ni miti ya wastani , vikonyo havipo wazi kwa hiyo huwapa kazi waungaji (hawaipendi) ina uzao wa wastani na inakaribia ukame na matunda yake hayaivi haraka.

Upandaji.
Baada ya uungaji kukubali unaweza kuandaa shamba lako kwa kuchimba mashimo, kuweka mbolea na kusubiri msimu wa mvua, miche ipandwe mara tu baada ya mvua za kwanza kunyesha, umbali wa kupanda ni mita 8 * 8 kwa Jaffer na mita 5 * 8 kwa Valencia.

Palizi na matumizi ya mbolea.
Palizi ifanyike si chini ya mara 2 – 4 kwa mwaka na miche ikifikisha miaka 3 unaweza ukasafishia miaka mitatu unaweza ukasafishia visahani na kufyeka sehemu nyingine. Kwenye mbolea weka samadi iliyoiva debe moja hadi mbili kwa shimo, changanya mbolea na udongo wa kwanza kutoka shimoni, iwapo itatumika mbolea ya viwandani kama DAP, TSP, NPK na Mijingu Phosphate changanya mbolea hiyo na udongo wa juu wenye mboji (top soil).

Uzao.
Kuanzia miaka mitatu miche itaanza kutoa maua na kuzaa na huchanganya kuzaa baada yamiaka mitano, miche huendelea kuzaa hadi kufikia miaka mitano 25 – 30 tangu kupandwa.

Magonjwa na wadudu katika michungwa.

Magonjwa.
1.Vidonda katika shina.
Huletwa na aina fulani ya ukungu. Dalili za ugonjwa huu nikutokea sehemu ya shina ambayo hubadilika rangi.
Dalili; Huongezeka ukubwa na baadae kutoa utomvu.
Kudhibitisha; Hutokea sana sehemu iliyo na udongo ambao huatamisha maji.

2. Ugonjwa wa kukauka miti.
Husababishwa na virusi ambavyo husambazwa na chawa weusi.
Dalili; Sehemu ya shina hunyauka na ndani yake hutokea mipasuko pasuko,kasha mmea hudhoofika polepole na kutoa matunda madogo madogo, na majani hubadilika ghafla na kuwa ya njano.


3.Ugonjwa wa kutobadilika rangi kwa machungwa yanapokomaa.
Hutokea hasa kwenye sehemu za miinuko ya kati na kusambazwa na vidudu viitwavyo psyllids, na vile vile kwa kuchukua vikonyo na kubebeshea kutoka kwenye miti inayoonyesha dalili za ugonjwa.
Dalili; Hutokea mabaka ya njano kwenye majani, pia matunda huwa ya ukali nay a njano sana.
KUZUIA:
Sehemu ambazo ugonjwa unaweza kutokea angalia wadudu kama chawa. Hakikisha wadudu hawa hawashambulii miche kwenye kitalu. Wakiwepo, majani huonyesha kujikunja kwa kuweka mafundo sehemu ya juu. Vilevile epuka kuchukua vikonyo kutoka kwenye miti yenye dalili za ugonjwa huu.

WADUDU:

1.Nzi weupe (white fly).
Hawa ni wadudu ambao hukaa kwenye majani ya mimea wakizaliana na kufyonza virutubisho vya mmea, na hii husababisha mmea kudumaa na kutoa mazao duni.
Kuzuia:
Njia ya kiusalama zaidi ni kwa kupandisha shambani wadudu aina ya  Cales noacki ambao huwala hawa nzi weupe na kuzuia kusambaa kwao.

2.Wadudu mafuta (aphids).
Hawa ni wadudu weusi ambao hukaa kwenye majani ya mimea wakizaliana na kufyonza virutubisho vya mmea, nah ii pia husababisha mmea kudumaa na kutoa mazao duni.
Kuzuia:
Tumia kiuwa wadudu (insectside).

Kuvuna
Mchungwa huwa tayari kuvunwa miezi 3 – 4 baada ya kupandwa. Kuvuna ni kwa njia ya mikono au kwa kutumia kikapu cha kuvunia.

Hifadhi
Machungwa huhifadhiwa kwenye ghala safi lenye kuruhusu hewa. Ghala lijengwe nje ili kuruhusu hewa safi ili yasioze.




Soko
Soko la ndani na nje ya nchi lipo. Kiasi kikubwa cha machungwa hutumika hapa nchini, pia huuzwa nchi za jirani. Bei ya chungwa ni shilling 200 – 300 kwa kila moja na hadi 500 hufikia kulingana na aina ya msimu.


Hitimisho
Ili kupata mmea wa mchungwa kama tunda ambalo linanunuliwa, huna budi kuitunza mbegu hiyo kwenye unyevunyevu kasha tu baada yaya kuzitunza kwenye tunda na kuziotesha katikahali ya unyevu; na pindi mmea uchipuapo hapo ukapandwe kwenye udongo kusudiwa.

No comments:

Post a Comment