Sunday, October 7, 2018

KILIMO BORA CHA MAHINDI

 Image result for picture of maize plantImage result for picture of maize cob 

1.UTANGULIZI

Mahindi ni zao la nafaka ambalo lina kiasi kikubwa cha wanga.Kwa kiasi kikubwa mahindi hulimwa kama zao la chakula,lakini pia likilimwa vizuri linaweza kutumika kama zao la biashara kutokana na mavuno yake mazuri,Ekari moja hutoa Kg 2000 hadi 4000 kutegemea na matunzo na aina ya mbegu.
2.HALI YA HEWA IFAAYO
Mahindi huwezwa kulimwa na kustawi vizuri katika uwanda wa chini kutoka usawa wa bahari hadi mwinuko wa mita 2500 kutoka usawa wa bahari.Mahindi mengine hukubari vizuri katika ukanda wa chini na mengine katika ukanda wa juu.hukua vizuri katika maeneo yapatayo mvua za kutosha kiasi cha milimita 750 na kuendelea kwa mwaka hustawi katika nyuzi joto 22 -33 C.

3.ARDHI IFAAYO KWA KILIMO CHA MAHINDI

Hustawi vizuri katika udongo wenye rutuba ya kutosha na wenye pH ya 6 hadi 7.hukubari katika udongo wa aina tofauti tofauti usiotuamisha maji.unaweza kulima katika udongo wa kichanga au mfinyanzi japokuwa katika udongo wa mfinyazi kama mvua itakuwa kubwa na maji yakatuama kwa muda mrefu huzuia ukuaji mzuri wa Mahindi.

4.MAANDALIZI YA SHAMBA LA MAHINDI

Shamba la mahindi inabidi liandaliwe mapema kwa kulisafisha na kuondoa uchafu na takataka zisizoweza kuoza kwa urahisi,Kisha shamba lilimwe vizuri kabla ya msimu wa kupanda kuanza.Shamba hilo linaweza kulimwa kwa kutumia trekta Jembe la mkono au kukokotwa na ng'ombe.

5.MBEGU BORA ZA MAHINDI

Kuna aina mbali mbali za mbegu bora za mahindi,na mbegu hizi hufaa zaidi kulingana na ukanda husika kutokana na utofauti wa hali ya hewa na urefu au ufupi wa msimu wa mvua
Maeneo ya nyanda za juu kusini hupata mvua nyingi na za muda mrefu katika msimu hivyo mbegu nyingi za hybrid hufaa katika kanda hizi mikoa ya nyanda za juuu inajumlisha Mbeya,Iringa ,Rukwa n,k na Mikoa ya nyanda za chini hupata mvua chache na za muda mfupi kama vile Dodoma,singida na mikoa mingi ya sehemu za pwani kama vile Lindi,Mtwara na Tanga.

AINA ZA MBEGU.
 Mbegu aina ya chotara(hybrid)-Hufaa katika maeneo yenye mvua nyingi mfano UYOLE, DK,SIDCO ,PANNAR, PIONEER, KITALE

 Aina ya ndugu moja(synthetic)
 Mbegu aina ya composite-Hufaa maeneo yenye mvua chache mfano TMV 1,TMV 2,staha,Kito.Katumbili n.k
Mbegu za kisasa zikitumiwa vizuri katika vizuri katika misingi ya kilimo zina uwezo wa kuzaa magunia 20-40 kwa ekari.

6.UPANDAJI WA MAHINDI

Mahindi inapaswa yapandwe mwanzoni mwa msimu wa mvua,ili yaweze kukua vizuri na kutoa mavuno yaliyo bora.
Kiasi cha kilogram 7- 10 za mbegu ya mahindi huitajika katika ekari moja.

NAFASI YA UPANDAJI
Fukia mbegu yako katika kina cha sentimeta 2.5 hadi 5 ardhini.
kuna nafasi mbalimbali za upandaji wa mahindi kama vile 
sentimeta 90 kwa 25- 30- mbegu moja moja
sentimeta 90 kwa 40- 50 Mbegu mbili
sentimeta 75 kwa 30 mbegu moja 
sentimeta  75 kwa 50 Mbegu mbili au 
sentimeta 80 kwa 40-50 kwa mbegu mbili.


MUDA WA KUPANDA

Maeneo mengi hupandwa mapema kuanzia mwezi wa  Novemba hadi Januari. kulingana na unyeshaji wa mvua za msimu.Kupnda mwanzoni mwa mvua ni bora zaidi.

FAIDA ZA KUPANDA MAPEMA

Mahindi yanapata mvua ya kutosha hadi kukomaa.
    Magonjwa kama yale ya ya majani (streak ugonjwa wa milia) hayatatokea au yatakuwa kidogo.
Mbolea uliyoweka itayeyuka pamoja na mahindi yastawi vizuri.

Image result for picture of maize plant



7.PALIZI NA KUPUNGUZA MIMEA KATIKA MSTARI.

Kama shamba lako lina magugu mengi hakikisha unapalilia mapema kabla mimea haijazidiwa na magugu.katika kila shimo hakikisha unabakisha miche miwili ya mimea ya mahindi.hakikisha shamba lako linakuwa safi muda wote.

8.MBOLEA.

Mahindi hukubari vizuri katika maeneo yenye kiasi kikubwa cha rutuba katika udongo,hivyo ili upate mavuno mengi ya mahindi utahitajika upande katika shmba lenye mboji au samadi au shamba lako uwe unatumia mbolea katika upandaji na ukuaji wa mimea.
Unaweza kutumia mbolea za asili kama vile mboji,samadi au  mbolea ya majani ya miti.-Hizi zina kiwango kidogo cha virutubisho.

MBOLEA ZA KUPANDIA MAHINDI
Pia unawza kutumia mbolea za viwandani katika kupanda kwa kiasi cha kg 50 kwa ekari ,mbolea kama vile DAP,Minjingu mazao,NPK au DSP kulingana na upungufu wa virutubisho vya aina fulani katika udongo.Mbolea  za kupandia huwekwa katika shimo la kupandia kabla ya kuweka mbegu (baada ya kuchimba shimo unaweka mbolea gram 5 kisha unafukia kidogo na kupanda mbegu yako na kufukia Tena,

MBOLEA ZA KUKUZIA MAHINDI
Mbolea za kukuzia kama vile N.P.K,UREA ,CAN,SA hutumika katika kukuzia mimea na kuzalishia mbegu kwa kiasi cha kg 50 kwa ekari.
Mbolea hizi huwekwa baada ya palizi ya kwanza  ambayo hufanyika kati ya wiki ya 3 hadi 4 tangu mahindi kupandwa shambani.Kwa maeneo ambayo mahindi au hupandwa mbegu ambayo huchukua muda mrefu zaidi kukomaa zaidi ya miezi 3 na 4 inashauriwa kuweka mbolea za kukuzia mara mbili.Mara ya kwanza mbolea huwekwa mwezi wa kwanza  baada ya kupanda na  mbolea hurudiwa tena kuwekwa yakifikia  mwezi 1 na nusu (siku 45) hadi Miezi 2 (siku 60). Pia kwa ziada unaweza ukaweka kwa Mara ya tatu Kg 12.5 kwa ekari mbolea ya kukuzia Mara baada ya mahindi kuanza kubeba,Lengo la uwekaji wa tatu wa mbolea ni kuhakikisha jani linalolisha hindi(flag leaf) linakuwa la kijani hivyo kupata mavuno zaidi.
Jinsi ya kuweka mbolea hizi-Kuzungusha shina kwa mbolea bila kugusa mmea,Kuweka mbolea kwa vifungu viwili au zaidi kuzunguka mmea. 
KUMBUKA-Haitakiwi kurundika mbolea sehemu moja,Haitakiwi mbolea hizi kugusa mmea wakati wa kuweka kwani zina kiasi cha chumvichumvi ambacho kinaweza kuathiri mmea kama hakuna unyevu wa kutosha.

PIA-MKULIMA lazima ajue kuwa mbolea hizi huwekwa wakati udongo una unyevu wa kutosha au kuna dalili za kunyesha kwa mvua ili kuwezesha mimea kuitumia kwa urahisi bila madhara na Pia kuzuia mbolea isipotee kwa jua kali.

9.UMWAGILIAJI

Kama mvua zitakuwa ni tatizo unaweza kuyamwagilia mhindi yako maji kwa kuangalia kutozidisha hali ya maji katika shamba lako

10.WADUDU 
WADUDU WAHARIBIFU WA MAHINDI 

A) Viwavi Jeshi
 Ni wadudu aina ya funza ambao hutokana na Nondo.Hushambulia mahindi kwa kula majaniyake pamoja na shina. 
Wadudu hawa huangamizwa/kudhibitiwa kwa njia zifuatazo;-
 Kuondoa vichaka karibu na shamba
Kunyunyizia sumu za asili kama vile Mwarobaini majuma mawili ya mwanzo.
Kunyunyizia sumu za viwandani endapo wadudu wameanza kuonekana kama vile Karate au DUDUALL au DUDUBA

B) Funza wa Mabua (Maize Stalk Borer).

Image result for picture of maize plant with maize stalk borer
    Funza wa mabua hutoboa shina la mahindi na kusababisha kudumaa kwa mahindi.
    Matundu, ungaunga kama wa msumeno huonekana kwenye majani yaliyoathiriwa.
    Mashambulizi huanza juma la pili hadi la tatu baada ya mahindi kuota.

Njia za kudhibiti zinazotumika
    Kuchanganya mahindi na mazao jamii ya mikunde kam vile maharagwe
    Kung oa mahindi yaliyoshambuliwa

TIBA
    Puliza Sumu za asili mwarobaini au 
    Sumu za viwandani kama vile Karate au Duduall au duduba

KUMBUKA -Unapopuliza dawa hakikisha maji  maji ya dawa yameingia ya kutosha katika mirija ya majani ya katikati ya mahindi.

10.UVUNAJI WA MAHINDI

Mahindi huvunwa .Mahindi huchukua siku  au miezi 4 hadi 6.Kupandwa na kukomaa.Mahindi yaliyokommaa mimea yake huanza kukauka  maganda ya nje .Mahindi huvunwa kwa kifaa maalum ya kuvunia au kuvunwa kwa mikono.Kisha hukaushwa vizuri na kupukuchuliwa kwa mashine au mikono ili kutenganisha na vigunzi/vibunzi vyake. Kisha yaweke katika magunia tayrai kwa kuhifadhiwa.

12.UHIFADHI WA MAHINDI

Baada ya kupukuchuliwa mahindi huwekwa katika mifuko kama vile viroba au magunia na kuwekwa gharani kuhifadhiwa.Mahindi huifadhiwa gharani baada ya kuyachanganya na dwa za kukinga na kuu wadudu kama vile actellic super Dust (SHUMBA) n.k Pia kuna mifuko maalum ya kuhifadhia mahindi ambayo huwezesha kulinda mahindi yasishambuliwe na wadudu.

No comments:

Post a Comment