Sunday, October 7, 2018

MAEMBE NI UTAJIRI MKUBWA

Waswahili husema eti rizizki ya Mbwa ipo miguuni mwake,usemi huu unamaana kuwa riziki ya mtu ipo katika nafasi aliyo nayo na uwezo alionao
Maembe yaliopo Tanzania yanaweza kubadilisha na kumuongezea riziki ya mkulima wa Tanzania kama akielimishwa vizuri kuhusu ukulima bora na wa kisasa
Maembe yanaweza kumnyanyua mkulima kwa kumuongezea kipato na kuboresha maisha ikiwa ni pamoja na kukuza uchumi wa nchi.
Utayarishaji wa shamba la miembe,mkulima anashauriwa kuandaa shamba mapema, kutumia mbegu na miche bora iliyofanyiwa utafiti na vituo vya utafiti hapa nchini.
Mikoa yote inalima miembe ila inatofautiana kwa kiwango cha uzalishaji kutokana na tofauti za maeneo hayo
Zao hili linalimwa katika mikoa yote kwa sababu ya uwezo wake wa kustawi katika aina mbalimbali za udongo na kustahimili aina mbalimbali za hali ya hewa ikiwa ni pamoja na ukame.
Miembe inaweza kustawishwa mahali ambapo aina nyingine nyingi za mazao haziwezi kustawi.
Zanzibar ilishazalisha jumla ya Tani 6,546. Kiasi hicho cha embe kilivunwa katika mashamba yenye jumla ya eneo la Hekta 1,372
Ingawa miembe imepandwa Zanzibar katika eneo lenye jumla ya Hekta 1,734 na kaya zilizohusika na kilimo hiki ni 12,819.
Ingawa takwimu hizo hazikuonesha kuwa sasa Tanzani iko nafasi ya ngapi katika uzalishaji wa zao la embe ,
Hata hivyo zinaonesha kuwa kuna ongezako la Tani 146,028 katika kipindi hicho. Ambapo maembe mengi yamezalishwa hapa Tanzinia
Soko la maembe limekuwa kwa kiasi kikubwa duniani ikiwa ni moja ya sababu ya kuongezeka wataalamu wa maembe
Kuna aina zaidi ya 140 za embe ambazo hupatikana hapa tanzania na duniani kwa ujumla kulingana na mazingira yake
.
Ubora wa embe unatofautiana kutokana na sifa za embe na aina ya embe husika ijapokuwa kila embe lina ubora wake.
Sifa hizo zipo nyingi sana, hata hivyo ili kurahisisha kuzitofautisha baadhi ya embe zinazojulikana zaidi katika masoko Tommy Atikns KEITT na kent zill aina hizi ni nzuri sana
Hukomaa mwanzoni hadi katikati ya msimu Matunda yake ni makubwa, huweza kufikia kati ya gramu 450 hadi 700 Umbile la tunda ni kati ya umbile la yai na mviringo
Likikomaa huweza kukaa muda mrefu bila kuharibika Tunda lina rangi nyekundu ambayo haijakolea na imechanganyika na njano na Lina utamu wa kadiri
Zipo aina nyingi za maembe zilimwazo na wakulima hapa nchini kama vile embe dodo, bolibo, sindano, zafarani, mviringa na nyingine nyingi ambazo tumezizoea.
Aina hizo za maembe uzalishaji wake ni mdogo lakini wataalamu wameweza kuingilia kati tatizo la uzalishaji mdogo kwa kutumia mbinu ya ubebeshaji wa maembe.
Ubebeshaji wa maembe ni njia sahihi katika kuhamisha sifa halisi cha maembe kutoka kwenye mche unaotoa mavuno mengi bila kuathiri sifa na tabia za embe unalokusudia kupata.
Mbinu hiyo hutumia shina mama lenye sifa ya kutafuta chakula kwa wingi ardhini na hubebeshwa na aina nyingine inayokidhi mahitaji ya mkulima kwa kumpa bei nzuri.
Matokeo ya utumiaji wa mbinu hiyo ya ubebeshaji wa maembe sasa kuna aina mpya za maembe zinazoweza kupenya soko la maembe la kimataifa.
Aina hizo ni Red, Apple, Alphoncal ambazo tayari zimepiga hodi kwa wakulima wa maembe wa wilaya ya Mkuranga.
Mbali na hayo kuna aina ya miembe inayokidhi sifa hizo ni pamoja na Kent, Keith, Tommy Atkins, Alphonso, Sabre, Van Dyke, Apple, Ngowe na Red Indian (Zill).
Wakulima walio karibu na bustani zinazomilikiwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika pamoja na zile zilizoko chini ya manispaa wameanza kupanda aina mpya za maembe.
Bustani zinazomilikiwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kupitia kitengo chake cha promotion ya mazao zipo Mpiji wilaya ya Bagamoyo mkoa wa Pwani,
Bustani ya Manispaa Ilala yenye aina mpya za maembe ni ile ya Kinyamwezi ambayo ipo nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam kupitia Gongola Mboto kuelekea njia ya Chanika,Pia zipo nyengine ambazo zipo maeneo ya Lushoto na Muheza Tanga
Wakulima wengi hawajui kanuni bora za kilimo cha maembe na hivyo kuwafanya wakulima kutoyaona manufaa ya maembe
Tatizo kubwa linalo kabili uendelezaji wa zao la embe ni kutopatikana kwa miche ya kutosha ya miembe bora.
Pia bei kubwa ya miche ambayo, huuzwa kati ya shilingi 2,000/= na 3,000/= kwa mche
Ili kuondoa tatizo la upatikanaji wa miche bora ya miembe Wizara ya kilimo chakula na ushirika imeweka mkakati wa kuongeza uzalishaji wa miche hiyo na upatikanaji kwa wakulima.
Miche hiyo bora ina sifa za kuzaa maembe mengi kwa eneo na yenye ubora unaokubalika katika masoko yetu ya humu nchini na yale ya nje ya nchi.
Wapo wakulima ambao wanawezeshwa kuanzisha mashamba ya miembe bora kwa kupewa miche bora ya miembe na kupanda katika mashamba yao.
Miembe imepandwa katika mikoa ya Pwani, Morogoro na Dodoma na sehemu nyingine hapa nchini.
Mashamba hayo yanakuwa ni mashamba ya mfano ambapo wakulima wanayatayarisha mashamba kwa kufuata kanuni zote za kilimo bora cha miembe.
Mashamba hayo yatakuwa ni sehemu ya kuwafundishia wakulima wengine kwa kuona aina mbalimbali za miembe bora jinsi inavyoweza kuzaa maembe yenye ubora zaidi
Baada ya miaka mitatu miche hiyo itaanza kuwa tayari kutoa vikonyo ambavyo vitatumika kuzalisha miche mingine unaofanywa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika katika kuendeleza zao la embe.
Jumla ya miembe bora 5,141 imezalishwa na kupandwa katika maeneo mbalimbali hapa nchini ili kuwafaidisha wakulima
Miche 595 ya miembe bora imepandwa Dodoma Vijijini huko Chamwino katika Tarafa ya Mvumi na vijiji vake, Makulu miche 200, Ilolo miche 100, Muungano miche 100 na miche 195 ilipandwa Ikowa Dodoma.
Pia Miche 150 imepandwa katika Kituo Cha Amani kijiji cha Makang’wa Dodoma,Miche 120 na kijiji cha mwambaya wilayani Mkuranga
Pia wapo wkulima ambao watagaiwa Miche mingine 400 wilayani Mkuranga namiche 250 itakayo gaiwa Morogoro.
Hata hivyo jumla ya Miche 3,500 ya miembe bora imezalishwa na Wizara ya Kilimo Chakula na Ushika kwa kushirikiana na wanachama wa Chama cha Wakulima wa Miembe ili kuwanufaisha wakulima
Miche hii ya kisasa inachukua miaka miwili na nusu kuanzia kupanda hadi kuzaa ile ya zamani inayochukua miaka mitano had saba kupanda hadi kuzaa
Kila mwaka idadi hiyo ya miche itakayozalishwa itakuwa inaongezeka kwa zaidi ya mara mbili Mashamba hayo ni ya wakulima wenyewe ambapo yanakuwa na malengo makuu matatu yafuatayo
Kama wakulima watatilia mkazo kwenye zao hili kwa kutumia mbegu sahihi za maembe zinazo zaa sana na kuchukua mda mfupi wanaweza kuondokana na umasikini
Mkoa wa pwani hivi karibuni uliweza kujionea mradi wa maembe ulikuwa umetembelewa na Raisi Jakaya Kikwete unaomilikiwa na Dkt. Salum Diwani
Shamba lililokuwa limesheheni miembe mingi ya kisasa iliyokuwa imezaa vizuri ilikuwa ni changamoto kwa yeyote alikuwepo kwenye mkutano huo kulima maembe
Iliwekwa wazi kuwa soko la maembe hayo linapatikana nchini Tanzania na nchi za jirani kulinga na ubora wake
Raisi Jakaya Kiwete alitoa changamoto kwa wizara ya kilimo chakula na ushirika kuandaa program maalum kuendeleza kilimo cha maembe katika mikoa inapostawi
Ilikadiriwa kuwa mti mmoja mkubwa wa mwembe huweza kutoa maembe hadi 3000 na midogo hutoa maembe 300
Huu ni utajiri kwani mkulima akilima miti kumi ikazaa vizuri midogo inaweza kuzaa maembe elfu tatu 3000 na mikubwa kutoa maembe elif thelathin 30,000
Hivyo mkulima akiuza embe moja kwa shilingi 300 huweza kupata kati ya 900’000 na 9,000,000 kwa miembe mikubwa na midogo
Mkulima angeweza kufaidika sana na kilimo cha maembe na hata kuitambulisha nchi kimataifa
Kuna mradi ujulikanao kama common Fund for Commodity ambao Tanzania na Zimbabwe ni wanachama na wamepewa furusa ya kuandaa mazao ya biashara ya kuuza nchi za nje
Soko la miembe hapa Tanzania lipo isipokuwa wanunuzi kutoka nje wanahofia kufanya biashara na watanzania kwa kile wasemacho kuwa hawjajipanga kutojitosheleza
Wenyewe
Yupo Inzi ajulikanaye kama inzi maembe kwa jina la kitaalamu bactrocera invadens husababisha funza ambao huharibu maembe
Funza anayejitokeza baada ya mayai kuanguliwa huishi kwa kula nyama ya maembe na kusababisha vidonda ndani ya embe na matokeo yake ni kuoza kwa embe.
Mara nyingi funza huchangia kwa kiasi kikubwa kushusha thamani ya embe na kufanya soko lake kuanguka
Wadudu wanachangia kuharibu soko la embe kutokana na kufanya embe kuoza mapema kabla ya kuiva na kupelekwa sokoni
Wapo wadudu mbalimbali ambao wanaweza kuharibu maembe kama vile Inzi ambao hutoboa na kutaga mayai ndani ya embe na husababisha embe kudondoka mtini
Tuna wakulima wengi wa maembe sehemu nyingi hapa Tanzania kama Kilimanjaro Tanga na hata Morogoro ambapo mda sio mrefu watakuwa na elimu kuhusu kilimo cha maembe
Ijapokuwa sio wakulima wote wana elimu kuhusu kilimo endelevu cha maembe na magonjwa yanayo athiri zao la maembe lakini elimu hawezi kuwa kuta wote kwa wakati mmoja
Watalaam wa Wizara pamoja na wa Halmashauri huvitembelea vijiji mbalimbali na kukutana na serikali ya kila kijiji husika ili kuwaewesha kazi inayokusudiwa kufanyika katika vijiji vyao.
Katika hatua zote ushirikishwaji wa wakulima unazingatiwa ili kukifanya kilimo hiki kuwa endelevu.Ili kutimiza azma hiyo Wizara imekwisha fanya mabo mengi mfano
Wizara imekiimarisha Bustani ya kuzalisha miti ya matunda ya Mpiji huko Bagamoyo pamoja Pampu za maji 5 ambazo zimenunuliwa.
Matenki ya maji 5, moja la lita 3,000 na manne ya lita 2,000 kila moja yamenunuliwa ili kukizi mahitaji muhimu.
Watanzani tuna takiwa kuiga mfano wa Colombia ambayo huwa inapata dola za marekani mill.200 kwa mwaka kwa kuuza maembe Ulaya pesa ambayo kwa Tanzania ni sawa na mazao mawili
Ili kufikia lengo la kukuza soko la maembe kwa, mkulima anatakiwa kupalilia shamba lake pamoja na kusambaza dawa za mda mfupi
mwisho

No comments:

Post a Comment