UTANGULIZI
Matikiti
maji hulimwa kama zao la biashara katika sehemu nyingi duniani zenye
hali ya hewa ya joto la wastani. Zao hili lina wapatia watu shughuli za
kufanya na hivyo kuwapatia kipato kuanzia kwenye nyanja za uzalishaji
hadi kwenye matumizi. Matikiti maji ni mojawapo ya jamii aina ya matunda
au mbogaboga inayotambaa. Mimea hii inapatikana katika kundi
linalojumuisha mimea mingine kama kama matango,maboga na maskwash. Zao
la tikiti maji ni mojawapo ya zao ambalo lina faida kubwa sana
ukilinganisha na mazao mengine kwa muda mfupi.
Katika
shamba la ukubwa wa shamba la ekali moja(1.acre) lililoandaliwa vizuri,
kupandwa na kuhudumiwa vizuri mkulima ana uwezo wa kuvuna kiasi cha
TANI 15-36, ambacho kitamsaidia kupata fedha zitakazo msaidia katika
mahitaji yake mbalimbali na kuondokana na Umasikini.
HALI YA HEWA
Mimea
hii husitawi katika maeneo yenye joto la wasitani yaani haihimili hali
ya joto kali sana,baridi kali, mvua nyingi na udongo unaotuamisha maji,
magonjwa ya fangasi na wadudu waharibifu. Matikiti hukua vizuri katika
maeneo yenye joto la wastani wa nyuzi kati ya 21-30 sentigradi. Iwapo
mitikiti itapandwa katika maeneo yenye joto chini ya nyuzi 15 za
sentigrade huchelewa kuota
Mvua
: kwa upande wa mvua matikiti yanahitaji kiasi cha mvua kati ya
millimita 400-600 kwa msimu. Mvua nyingi husababisha uwepo wa magonjwa
ya fungusi na bakiteria ambayo huathili mavuno.
Hali ya Udongo
Huhitaji
udongo wenye rutuba nzuri ulio na virutubisho. Vile vile haihitaji
udongo wenye kiasi kikubwa cha tindikali na alikali kubwa. Hali ya
udongo kipimo cha pH iwe kati ya 6.0 na 7.0. Ingawa mmea una uwezo vile
vile wa kuhimili kwenye udongo wenye pH 5.0
MAENEO YANAYOFAA KWA KILIMO CHA MATIKITI MAJI TANZANIA.
Kwa
upande wa Tanzania Inastawi vizuri kwenye ukanda wa pwani na miinuko
kidogo kama DSM,Tanga, Morogoro, Mtwara, lindi na Pwani ambapo kuna jua
la kutosha. Muda mzuri wa kupanda ni kipindi cha kipupwe mwezi wa tatu
mpaka wa tisa.
UANDAAJI WA SHAMBA
Kabla
ya kupandikiza udongo utifuliwe vizuri na majani yaondolewe
kabisa.Shamba liandaliwe vizuri kwa kusafisha ili kuondoa mimea mingne
ambayo inaweza kuwa ni chanzo cha magonja.
UPANDAJI
Katika
shamba la ukubwa wa hecta moja kiasi cha kilo 3-4 cha mbegu kinaweza
kutumika. Panda mbegu 2 au 3 moja kwa moja katika kila shimo. Usipande
katika kitalu kwasababu miche ya mitikiti huwa ni dhaifu sana wakati wa
upandikizwaji iwapo itapandwa kwenye kitalu hivyo kupelekea kufa kwa
miche hiyo. Panda umbali wa sentimeta 2 chini ya udongo kwa umbali wa
sentimeta 30 kutoka shina hadi shina na mita 1.5 - 2 kutoka mstari hadi
mstari. Zingatia kutokutumia mbegu za tikiti uliloninua kwasababu
linaweza kuwa ni chotara (Hybrid) ambayo hupelekea kushusha kiasi na
ubora wa matikiti yatakayo zaliwa kwa sababu yatakuwa ni kizazi cha pili
(F2)
UPUNGUZAJI WA MIMEA
Mimea
ya michikichi huanza kuota, baada ya kama wiki 2. Hivyo katika Mbegu
mbili ulizopanda kata moja na uache ule mche wenye afya zaidi ndio
uendelee kukua.
Aangalizo
using’oe mche bali ukate ili kuzuia kusumbua mizizi ya mche uliobaki.
Vilevile unaweza kupandishia udongo kwenye mashina ili kusaaidia
kupunguza maji kutuama kwenye mimea yako, pia unaweza kuweka samadi
badala ya kupandishia udongo ukiwa na nia ileile ya kuzuia maji
yasituame na kuongeza rutuba.
Kama
una sehemu ndogo ya shamba unaweza kuyawekea matikiti waya ya
kutambalia, ila inabidi uwe imara kwa sababu ya kuhimili uzito wa
matunda.
Wakati mimea inapo anza kutambaa kwenye waya ni lazima uifundishe (kuielekezea ) kwenye waya na kuifungia.
MATANDAZO (MULCHES
Matandazo
ina maana ya kutumia nyasi na mabaki ya mimea mingne kufunika aridhi.
Baada ya miche kutambaaa kwa kiasi unaweza kuweka matandazo (mulches)
ambayo yaweza kuwa nyasi kavu kwenye udongo ili kuzuia upotevu wa unyevu
vile viile kupunguza uotaji wa magugu shambani kwako. Vile vile
matandazo yakioza yanaongeza rutuba kwenye udongo na hulinda udongo
dhidi ya mmomonyoko wa udongo.
UWEKAJI WA MBOLEA
Mbolea
za viwandani aina ya NPK au mbolea zenye nitrogen kiasi cha gram 10
hadi 20 ziwekwe wakati mimea ikiwa ni midogo mpaka pale maua ya kike
yatakapoanza kuonekana. Vilevile samadi inaweza kuwekwa wakati mimea
ikiwa midogo. Baada ya mimea kutengeneza matunda weka mbolea aina ya
urea na potassium hadi mara 2 au 3 kwa wiki mpaka matunda yatakapokomaa.
UMWAGILIAJI
Shamba
linatakiwa limwagiliwe mara kwa mara wakati mvua zinapokosekana au
wakati wa mvua chache. Kipindi muhimu zaidi ambapo mimea hii huhitaji
maji ni katika kipindi cha uotaji wa mbegu, wakati wa kutoa maua na siku
takribani kumi kabla ya kuvuna. Iwapo kutakuwa na ukosefu wa maji
kutasababisha kutengenezwa kwa matunda ambayo si mazuri na yenye umbo
baya wakati wa utengenezaji wa matunda pia upunguaji wa ukubwa wa tunda.
Angalizo;
usimwagilie matikiti wakati wa jioni sana au usiku kwasababu inaweza
kusababisha magonjwa ya majani kutokana na unyevu kukaa muda mrefu. Vile
vile usimwagilie juu ya maua wakati wa asubuhi au join kwasababu
unaweza kuzuia wadudu kama nyuki ambao ni muhimu sana wakati wa
uchavushaji.
MAUA NA MATUNDA
Matikiti
hutoa maua dume na jike kwenye tawi moja. Kwa kawaida maua dume huwa ni
madogo zadi na hutoka mapema zaidi yakifuatiwa na maua jike ambayo huwa
makubwa zaidi. Maua yanaweza yasionekane au yasitokee iwapo kiasi
kidogo cha maji kitamwagiliwa ,upungufu wa viritubisho kwenye udongo na
hali ya hewa ya joto/baridi sana n.k
Uchavushaji hufanya na wadudu na iwapo itaonekana hakuna wadudu unaweza kuchavusha kwa kutumia mkono.
Hii
hufanywa kwa , kukata maua dume kwa kisu na kufanya uchavushaji kwenye
maua jike, maua jike ya mwanzo kwenye tawi ndiyo yenye ukuaji bora
zaidi, unaweza kukata tawi lisiendelee kukua baada ya matunda kutokeza
hii husababisha kuwa na matunda makubwa zaidi. Hii inawezwa kufanywa
zaidi wakati wa Asubuhi.
MAGONJWA NA WADUDU
Wadudu
wa matikiti wako wa aina mbalimbali na wanaoshambulia sehemu
wanaoshambulia majani na maua, na wengine hushambulia matunda , pia kuna
magonjwa ya fangasi ambayo hushambulia mimea. Magonjwa kama Ukungu wa
unga (powdery mildew) na wa chini (Downy mildew) na mengine yathibitiwe
kabla hayajaleta madhara kwenye mimea.Ili kujua dawa za magonjwa ni
vizuri kuchukua sampuli na kwenda nayo kwenye duka la dawa na pembejeo
za kilimo ili kupata dawa sahihi. Dawa aina ya Mancozeb inaweza kutumiwa
kuthibiti ugonjwa magonjwa hayo hapo juu.
Vilevile matikiti hushambuliwa na wadudu ambao hukaa katika majani, maua na matunda.
Dawa aina ya KARATE itasaidia kuua wadudu wa majani, maua na matunda.
UVUNAJI MATIKITI
Kabla
ya kuvuna matunda ni vema kwanza kujua kuwa matikiti huchukua takribani
miezi mitatu mpaka mitano toka inapopandwa mpaka kukomaa. Hii hutegemea
na aina ya matikiti yenyewe. Tikiti lililo komaa linaatakiwa na
mwonekano wake huwa kama ifuatavyo;
Rangi ya mng’ao hupotea
Upande wa chini wa tunda huanza kuwa na rangi ya njano
Pia kikonyo juu ya tunda hukauka kabisa na kuwa kijivu.
Ila njia nzuri ni kuyapiga kwa kiganja na kusikiliza mlio wake unakuwa kama mlio wa ngoma.
Tumia kisu wakati wa kuvuna matikiti, yabebwe na kuhifadhiwa vizuri kwenye makasha tayari kuuzwa au kwa matumizi binafsi
Soko la matikiti maji
Ukubwa
wa tikiti na mwonekano wake ni baadhi ya sifa zinazoangaliwa na
wananuzi. Matikiti madogo sana huwa hayapendi sana na wanunuzi. Kwa
Tanzania wakulima wengi wanauza matikiti katika masoko ya ndani
yanayopatikana takribani nchi nzima. Kwa miaka kadhaa tikiti moja
limekuwa likiuzwa kwa wasitani wa shilling 1000 kwa tikiti dogo mpaka
3000 kwa tikiti kubwa katika masoko.
Mavuno
Mavuno
ya matikiti yanategeme huduma za shamba pamoja na hali ya hewa.
Matikiti pia hutofautiana katika mavuno kulingana na aina ya matikiti.
Kwa wastani matikiti yanaweza kutoa kutoa mavuno kati ya TANI 15-36 kwa
hekta moja.
Asanteni saana kwa elimu hii
ReplyDeleteNimepata pa kuanzia
Asanteni saana kwa elimu hii
ReplyDeleteNimepata pa kuanzia
Aksante kwa Elimu hii.
ReplyDelete