Hili ni zao la biashara, pia chakula. Zao hili hustawi na kulimwa kwa wingi katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga na Pwani.
Matumizi: Matango
hutumika kama tunda, ijapokuwa ni aina ya mboga na huongeza vitamin A, C
na maji mwilini. Pia, tango linaweza kutumiwa kama saladi wakati wa
mlo.
Hali ya hewa: Matango
hustawi kwenye hali ya joto, hali kadhali kwenye sehemu yenye joto
kidogo pia hustawi. Matango yanahitaji joto wastani wa nyuzi joto 20°C –
25°C. Zao hili pia huhitaji maji kwa wingi, ingawa unyevu ukizidi
husababisha magonjwa kwenye majani na maua.
Udongo: Kwa
ustawi mzuri wa matango, udongo unatakiwa kuwa na rutuba ya kutosha, na
chachu ya kuanzia 5.5 hadi 6.7, mwinuko unaotakiwa ni kuanzia mita
1000-1200 kutoka usawa wa bahari.
Tofauti
na ilivyo mazao mengine, matango hayahitaji mwanga mkali sana kwa kuwa
husababisha maua dume kuzaliwa, hivyo kuathiri uzalishaji wa idadi ya
matunda ya matango. Mwanga kidogo husababisha maua jike kuchanua kwa
wingi kuongeza kiwango cha mazao. Mwanga unapokuwa mwingi, inabidi
kutumia neti au aina nyingine ya vizuizi ili kupunguza mwanga, ambapo
pia itasaidia kulinda mmea dhidi ya upepo mkali ambao unaweza kuharibu
maua na matunda, au mmea kwa ujumla.
Kupanda: Mara
nyingi matango hupandwa moja kwa moja shambani. Wakulima wengine
hupanda kwenye vitalu au makopo na baadae kuhamishia miche inapofikia
sentimita 8-12. Endapo mbegu zimepandwa shambani moja kwa moja,
inatakiwa ipunguzwe na kubakia mche mmoja tu kwenye kila shimo.
Nafasi: Nafasi
kati ya mche na mche ni sentimita 60-70, na nafasi kati mstari na
mstari ni sentimita 70-90. Mimea inatakiwa iwekewe miti ili iweze kuzaa
matunda mengi na kuepuka kukaa chini ambapo matunda yanaweza kuoza au
kuharibiwa na wadudu.
Mbolea: Mbolea
ni muhimu sana, kabla ya kupanda au kuhamisha miche. Mbolea inayoweza
kutumika ni samadi au ya viwandani isiyokuwa na madhara kwa mazingira na
afya ya binadamu. Baada ya kupanda, tumia mbolea ya maji maji kila
baada ya siku 14-21, mpaka mmea uweke matunda.
Palizi: Palizi ni muhimu , ili kuepuka magonjwa na kunyang’anyana chakula kati ya zao na magugu.
Wadudu waharibifu: Wadudu waharibifu wa matango ni pamoja na Vidukari, inzi weupe, na minyoo ya mizizi.
Magonjwa: Magonjwa yaliyozoeleka kushambulia matango ni pamoja na Ukungu, fusari, na magonjwa ya virusi.
Kuvuna: Matango
yanaweza kuwa tayari kuvunwa kuanzia siku 50-60 na matunda yanatakiwa
yawe na urefu wa sentimita 15 mpaka 20. Makadirio ya mavuno ni tani 6
kwa ekari moja.
Asante kwa hizo dondoo za kilimo cha Tango.Samahan naweza kupata details zaid za kilimo cha hili zao?
ReplyDeleteAsante kwa hizo dondoo za kilimo cha Tango.Samahan naweza kupata details zaid za kilimo cha hili zao?
ReplyDelete