Mahitaji ya hali ya hewa na udongo
Zao hili hupendelea hali ya hewa ya baridi na udongo tifu tifu na wenye rutuba. Sehemu
nyingi zinazostawi vitunguu maji hufaa pia kwa zao hili. Maeneo ya mwinuko wa kiasi
cha zaidi ya mita 1000 juu ya usawa wa bahari hufaa zaidi
Maandalizi ya shamba
Lima shamba kwa trekta, kwa ng’ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sen-
timita 30 hadi 45 Weka matuta ya mwinuko yenye upana wa mita 1 hadi mita 1.5 kutoka kati kati ya
tuta na tuta na upana wa mita 1
Maandalizi ya Mbegu
Kwanyua
vipande/Vikonyo vya vitunguu sumu tayari kwa ajili ya kupanda katika
nafasi. Mbegu sharti iwe imekaa kwa miezi mitano hadi sita tangu kuvuna
ili iweze kuota. Ni muhimu kwa mkulima kupata ushauri wa kitaalam ili
kujua namna ya kutam- bua mbegu ya vitunguu saumu iliyo tayari kwa
kupanda kwani ikipandwa kabla haijawa tayari haioti
Upandikizaji
Tumia
mashine alama kuweka alama za kupandia katika nafasi ya sentimita 15
hadi sentimita 25 na mistari minne hadi sita kwa tuta Hakikisha shamba
lina unyevu wa kutosha kabla ya kupanda
Palizi
Palilia
shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu Magugu
hudhibitiwa kwa palizi ya jembe, kung’oa kwa mkono ama matumizi ya
viuagugu.
Mbolea
Tumia
mbolea ya DAP wakati wa kupanda, CAN ama SA wiki tatu baadaye na kisha
tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji
yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji.
Matumizi ya viuatilifu
Matumizi ya viuatilifu yafanyike kila baada ya wiki mbili kwa ushauri wa wataalam
Mavuno
Vitunguu saumu hukomaa miezi 6 tangu kupanda
Bei ya mbegu hizi ni tsh 30,000/= kwa kopo la lita moja(1) na tsh 600,000/= kwa ndoo ya lita ishirini.
Guarantee:
Ndoo ya lita 20 ambayo ni sawa na makopo 20 ya lita moja inatosha
kupanda eneo la hekari 1 (m70*m70) na kiwango cha chini cha mavuno ni
gunia 100 na kiwango cha juu ni gunia 110-120 ndani ya siku 90 (3
months) toka kupanda. Gunia moja sokoni kariakoo, ilala, buguruni,
temeke na mabibo kwa sasa bei ni tsh 130,000/= * gunia 100 = tshs
13,000,000/= ndani ya miezi 3
Nimeipenda hiki kilimo he maeneo ya iring yaweza stawi kweli
ReplyDelete