Zao
 hili pia hujulikana kwa jina la "Nyanya Chungu", "Ngogwe" au "Ntongo". 
Huu ni mmea wa kitropiki, na kustawi kwake karibu ni sawa na bilinganya.
Mmea
 hukua na kufikia urefu wa meta moja hadi moja na unusu na matawi na 
majani yake hufanya kichaka. Nyanya mshumaa zinaweza kuwekwa katika 
makundi mawili: yaani aina itoayo matunda madogo madogo na machungu sana
 na aina itoayo matunda makubwa na machungu kidogo.
Rangi
 ya matunda huwa kijani kibichi au kijani-njano, au njano-nyeupe, na 
yakipevuka kabisa hugeuka mekundu. Matunda yafikia hatua ya kupevuka 
huwa hayafai tena kuliwa, ila kwa kutoa mbegu za kupanda. Matunda 
hupikwa au kukaangwa na kufanywa mchuzi, au huchanganywa na mboga 
zingine. Pia hupikwa pamoja na ndi.
Kupanda:
 Miche huoteshwa kwa kupanda mbegu ambayo husiwa kwenye kitalu na 
kutunzwa kama mazao mengine. Miche ifikiapo kimo cha sentimeta 10 hadi 
15 au majani manne 4 hupandikizwa bustanini , kwa umbali wa sentimita 50
 kwa 75 au  sentimeta 90 kwa 90, hadi 120 kwa 120; hii kutegemeana na 
ukubwa wa kichaka chake. Mimea ya "Ngogwe" hutunzwa kama bilinganya, 
huhitaji ardhi yenye rutuba na unyevu wa kutosha. Mazao huanza kuvunwa 
miezi miwili baada ya kupandikizwa, na uvunaji huendelea kwa muda mrefu 
kidogo.
Maadui:
 Nyanya Mshumaa ni mmea mgumu, kwani unaweza kustahimili upungufu wa 
maji kuliko aina nyingine za Mboga. Vile vile haushambuliwi sana na 
baadhi ya Magonjwa
yasababishwayo
 na mvua au uchepechepe mkubwa. Ingawa yako magonjwa na wadudu ambao 
hushambulia zao hili, madhara ya si makubwa sana kiasi cha kutisha au 
kumkatisha tamaa mkulima. Usafi wa bustani na kubadilisha mpando wa 
mazao, vinaweza kuondoa tishio hilo.
Kuvuna:
 Mboga huvunwa wakati zikiwa bado mbichi. Ili ziweze kukaa kwa muda 
mrefu (hata majuma mawili) bila kuharibika, inapendekezwa kuzichuma 
pamoja na sehemu ya vikonyo vyake. Vikonyo hivyo hukobolewa wakati wa 
kuzitayarisha kupikwa. Kwa hiyo, zao hili linaweza kusafirishwa hadi 
masoko ya mbali bila kuharibika.
Mkulima ongeza uzalishaji katika mazao ya mboga mboga ukuze uchumi wako.
NB:
 Umbali wa cm 50 kwa cm 75 ni mzuri sana kwa kuwa unaweza kupata mazao 
mengi na kupunguza wingi wa magugu ukizingatia in cover crop ila lazima 
uhakikishe ardhi yako ipo vizuri kwa rutuba maana matumizi ya mbolea ni 
amakubwa.


 
No comments:
Post a Comment