Bilinganya
imo katika jamii ya mimea inayohusisha nyanya, pilipili,
viazi mviringo na nyanya mshumaa. Mboga hii ina viini lishe
muhimu kama vile madini aina ya chokaa na chuma, Vitamini
A, B na C, wanga, protini na maji. Mboga hii hutumika
kutengeneza supu au kama kiungo katika vyakula mbalimbali.
Vilevile huweza kuhifadhiwa kwa kukatakata vipande na kuwekwa kwenye makopo.
MAZINGIRA:
Zao
hili huhitaji hali ya joto la wastani, udongo wenye kina
kirefu na rutuba ya kutosha na usiotuamisha maji. Kwa
kawaida bilinganya hulimwa zaidi ya msimu mmoja, lakini
katika nchi za Kitropiki (joto) zao hili hulimwa kwa msimu
mmoja.
AINA:
Aina za bilinganya zinazolimwa kwa wingi katika nchi za ukanda wa joto ni kama zifuatazo;-
Black Beauty:
Aina hii huzaa sana, matunda yake meusi, makubwa, na ya mviringo
Florida Market.
Matunda
ya Florida Market yana umbo la yai. Aina hii pia
huzaa sana, lakini hushambuliwa kwa urahisi na ugonjwa wa
mnyauko bakiteria (Bacterial wilt)
Florida High Bush.
Matunda yake ni makubwa yenye umbo la yai na rangi ya kijani kibichi iliyochanganyika na nyeusi.
Newyork Spineless.
Matunda ya Newyork Spineless ni ya mviringo, makubwa na yana rangi ya ya zambarau.
Peredeniya.
Aina hii huzaa sana, matunda yake ni makubwa kiasi na yana umbo la yai.
Aina
zingine za bilinganya ni matale, Kopek na Rosita. Aina
hizi huvumilia sana mashambulizi ya ugonjwa wa mnyauko
bacteria.
KUOTESHA MBEGU:
Mbegu
huoteshwa kwanza kwenye kitalu na baadaye miche
huhamishiwa shambani. Kabla ya kusia mbegu, tengeneza
tuta lenye upana wa mita moja na urefu wowote. Weka
mbolea za asili kama vile samadi au takataka zilizooza
vizuri, kiasi cha ndoo moja au mbili katika eneo la mita
mraba moja. Sia mbegu kiasi cha gramu mbili mpaka tatu
(nusu kijiko cha chai chenye ujazo wa gramu tano) katika
eneo hilo.
SOMA; Huu Ndiyo Ufugaji Rahisi Kwako, Unaoweza Kukutoa Kwenye Umaskini.
Gramu
500 za mbegu zinatosha kupandikiza katika eneo la hekta
moja. Nafasi kati ya mstari na mstari iwe sentimeta 10
hadi 15 na kina kiwe sentimita 1.5. Baada ya kusia mbegu
fukia na tandaza nyasi kavu na kisha mwagilia maji.
Endelea kumwagilia kitalu kila siku, asubuhi na jioni,
hadi mbegu zitakapoota. Mbegu huota baada ya siku ya 10
hadi 12.
KUHAMISHA MICHE:
Miche
huwa tayari kwa kupandikizwa shambani baada ya wiki sita
hadi nane. Wakati huu huwa na urefu wa sentimita 15
mpaka 20 (sawa na urefu wa kalamu ya risasi).
Mwezi
mmoja kabla kupanda miche, rutubisha udongo kwa kuweka
mbolea za asili zilizooza vizuri. Mbolea hizi ni kama
samadi, mbolea vunde na mbolea ya kuku.
Weka
kiasi cha tani 10 hadi 20 kwa hekta. Kiasi hiki ni
sawa na kuweka ndoo moja hadi mbili zenye ujazo wa lita
20 katika eneo la mita mraba moja. Mbolea ya mchanganyiko
aina ya N.P.K yenye uwiano wa 20:10:10 huwekwa kwenye
shimo wakati wa kupandikiza mche. Kiasi kinachohitajika ni
gramu tatu hadi tano (sawa na nusu kijiko mpaka kijiko
kimoja kidogo cha chai) kwa kila shimo.
Nafasi
ya kupandikiza hutegemea aina ya bilinganya. Aina ndogo
hupandikizwa katika nafasi ya sentimita 80 mpaka 100
kutoka mstari hadi mstari na sentimita 50 mpaka 60 kutoka
mche hadi mche. Aina kubwa hupandikizwa katika nafasi nafasi
ya sentimita 80 mpaka 100 kutoka mstari hadi mstari na
sentimita 80 mpaka 90 kutoka mche hadi mche. Kazi ya
kuhamisha miche ifanyike kwa uangalifu mkubwa ili kuepuka
kuikata mizizi.
SOMA;Badili Maisha Yako Kwa Kuwekeza Kwenye Kilimo Hiki Cha Vitunguu Swaumu.
KUTUNZA SHAMBA:
· Kuweka matandazo.
Mara
baada ya kupandikiza miche, tandaza nyasi kavu. Matandazo
husaidia kuhifadhi unyevu, huzuia magugu yasiote na
huongeza rutuba ya udongo.
· Palizi.
Hakikisha
shamba ni safi wakati wote ili kuzuia ushindani wa
chakula, maji na mwanga kati ya mimea na magugu. Usafi wa
shamba pia huondoa maficho ya wadudu waharibifu na huzuia
kuenea kwa magonjwa.
Mbolea.
Mbolea
ya kukuzia aina ya S/A huwekwa wiki tatu baada ya
mmea kuanza kutoa maua. Kiasi cha gramu tatu hadi tano
kuwekwa kuzungukia kila mche. Mbolea iwekwe katika
umbali wa sentimita tano mpaka 15 kutoka kwenye shina,
hutegemea ukubwa wa mche. Hakikisha mbolea haigusi mmea.
Kukata kilele.
Wiki
mbili baada ya kupandikiza miche, kata sehemu ya juu
ya mmea (kilele) kama umepanda aina ndefu ya bilinganya. Hii
itasaidia kupata matawi matatu hadi manne na mmea
kutengeneza kupata matawi matatu hadi manne na mmmea
kutengeneza umbile la kichaka. Matawi yakizidi manne
yaondolewe ili kupata mazao mengi na bora.
Kumwagilia.
Zao
la bilinganya hustawi vizuri likipata maji ya kutosha.
Umwagiliaji ufanyike kila siku asubuhi na jioni kutegemea
hali ya hewa.
Kuzuia Wadudu Waharibifu na Magonjwa.
Wadudu Waharibifu:
Vivyatomvu wa Bilinganya (Eggplant Lacebugs)
Wadudu
hawa hushambulia zaidi sehemu ya chini ya jani.
Hufyonza utomvu wa majani na kusababisha majani kuwa na
mabaka meupe au njano. Mashambulizi yakizidi majani
huanguka chini. Vinyatomvu wanaweza kuzuiwa kwa
kunyunyizia moja ya dawa zifuatazo;-
Deltamethrin (Decis), Dimethoate (Sapa Dimethoate) Fenvalerate (Sumicidin), Lambda - Cyhalothrin (Karate).
Vidukari au wadudu mafuta (Cotton Aphids)
Hawa
ni wadudu wadogo wenye rangi nyeusi. Hushambulia
majani machanga na kuyasababisha kudumaa na kukunjamana.
Zuia wadudu hawa kwa kutumia mojawapo ya dawa
zifuatazo;-
Dimocron 50% E.C, Lambda - Cyhalothrin (Karate) Dichlorvos (Nogos).
Utiriri wa Mimea (Red Spider Mites).
Ni
vidudu vidogo vyenye rangi nyekundu iliyoiva. Hushambulia
majani kwa kufyonza utomvu. Majani yaliyoshambuliwa
huonyesha utando kama wa buibui. Mashambulizi yakizidi
mea hudumaa, majani hukauka na hatimaye hufa.
Utiriri unazuiwa kwa kutumia dawa zifuatazo;- Acrex, Karathane 25% W.P, Dimethoate, Ekalux, Kelthane.
Minyoo Fundo (Root knotnematodes).
Wadudu
hawa hushambulia mizizi. Hutoa kinyesi ambacho ni sumu
kwa mmea. Sumu hii husababisha mizizi kuwa na nundu
kama ya mizizi ya maharagwe. Mashambulizi yakizidi mmea
hudumaa, hunyauka na hatimaye hufa.
Njia
ya kuzuia wadudu hawa ni kubadilisha mazao kwa mfano baada
ya kuvuna zao hili, zao linalofuata lisiwe la jamii moja
na bilinganya kama vile nyanya, pilipili na viazi mviringo.
Pia dawa aina ya Carbofuran (Furadan) inaweza kutumika.
Magonjwa:
Mnyauko Bakteria ( Bacterial Wilt).
Ugonjwa huu husababishwa na backteria. Mmea ulioshambuliwa hunyauka ghafla hasa wakati wa jua kali.
Mnyauko
bacteria unaweza kuziuwa kwa kubadilisha mazao shambani.
Endapo ardhi itashambuliwa na ugonjwa huu zao la
bilinganya lisipandwe katika eneo hilo kwa muda wa miaka
mitatu hadi mitano.
Njia
nyingine ni kupanda aina za bilinganya kama vile
Matale, Kopek na Rosita ambazo huvumilia mashambulizi ya
ugonjwa huu.
Phomopsis Vexans:
Ugonjwa huu husababishwa na bacteria na kushambulia majani, shina na matunda.
Verticillium Wilt.
Huenezwa na maji na husababisha mmea kudumaa, majani kukunjamana na kuanguka.
Magonjwa
ya Phomopsis vexans na Verticillium Wilt yanaweza
kuzuiwa kwa kung’oa ma kuchoma moto mimea
iliyoshambuliwa, kubadilisha mazao, na kuweka shamba katika
hali ya usafi wakati wote.
KUVUNA:
Bilinganya
huanza kutoa matunda yaliyokomaa baada ya miezi
miwili hadi mitatu tangu kupandikiza. Uvunaji huendelea
kwa muda wa zaidi ya miezi minne na hauna budi
ufanyike mapema mara matunda yanapokomaa. Matunda
yaliyokomaa sana hayafai kulimwa kwa sababu huwa na
kambakamba na mbegu zilizokomaa.
Vuna mara mbili au tatu kwa wiki, kwa kutumia kisu kikali ili usiumize matunda.
MAVUNO:
Kwa
kawaida zao hili huzaa sana iwapo limetunzwa
vizuri. Shamba lililotunzwa vizuri linaweza kutoa
mavuno tani 50 hadi 60 kwa hekta. Hata hivyo mavuno
mengi hutegemea aina ya bilinganya, umwagiliaji na rutuba
ya udongo.
No comments:
Post a Comment